MJEMA BLOG

JICHO LA MWANDISHI

  • RSS
  • Delicious
  • Digg
  • Facebook
  • Twitter

Picha ya Marehemu Meja Jenerali, Muhiddin Mfaume Kimario (76), aliyefariki dunia Oktoba 6, mwaka huu, katika Hospitali ya Apollo India alipokuwa amelazwa kwa muda mrefu akipatiwa matibabu, aliyezikwa Jana, Oktoba 11, mwaka huu katika makaburi ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Majeshi mstaafu, Meja Jenerali, Hagai Mrisho Sarakikya, akitia saini katika kitabu cha Rambirambi, Nyumbani kwa Marehemu, Meja Jenerali Muhiddin Kimario.
Mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM Taifa, Aggrey Mareale, akitia saini katika Kitabu cha Kumbukumbu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi mjini, Elizabeth Minde msibani hapo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kushoto, akijadili jambo na mkuu wa Majeshi mstaafu, Meja Jenerali Mrisho Sarakikya.
Mkuu wa Majeshi mstaafu, Meja Jenerali Mrisho Sarakikya, akitia saini katika kitabu cha Rambirambi.
Mkuu wa wilaya ya Rombo, Elinasi Pallangyo (aliyeinama) akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Meja Jenerali Mrisho Sarakikya.
Sheikh Salim Mubaraka kutoka Arusha akiongoza waumini na waombolezaji kusoma Talakini nyumbani kwa Marehemu Meja Jenerali Muhiddin Kimario.
Jeneza la Marehemu Meja Jenerali Kimario.
Wasanii wa Bongo Movie, Mzee Chilo (kulia) na Mzee Masinde nao walikuwepo.
Sehemu ya Waombolezaji.
Maofisa wa juu wa Jeshi la wananchi, akiwemo Meja Jenerali Ezekeil Kyunga (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa majeshi mstaafu, Meja Jenerali, Mrisakikya (wa pili kushoto), wakifuatilia taratibu katika mazishi ya Meja Jenerali mstaafu, Muhiddin Kimario.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akitia saini katika kitabu cha Rambirambi.
Heshima za kijeshi zilifuata
Msafara kuelekea msikiti wa Riadha kwa ajili ya kuuswali mwili wa Meja Jenerali Kimario
Umati mkubwa uliojitokeza katika msiba huo.
Jeshi la Wananchi ukifanya gwaride tayari kwa heshima za mwisho.
Mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu, Muhiddin Kimario ukiwasili katika eneo la makaburi.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika makaburi ya Manispaa ya Moshi, kushuhudia maziko ya Meja Jenerali Kimario, kulia kwake ni Mkuu wa majeshi Mstaafu, Meja Jenerali Mrisho Sarakikya na Kaimu Mkuuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi, kushoto kwake ni mkuu wa kikosi cha Batalion kanda ya Kaskazini, Meja Jenerali, Ezekiel Kyunga.
Ndugu wakijiandaa kuuhifadhi mwili wa Marehemu, Meja Jenerali Muhiddin Kimario.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mchanga kaburi la Marehemu Meja Jenerali Mstaafu, Muhiddin Kimario aliyefariki, Oktoba 6, mwaka huu na kuzikwa jana katika makaburi ya manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.DSC_0120
Mwalikishi wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii, Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo hicho cha redio jamii Uvinza FM uliofanyika wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Kutoka kushoto ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya, Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo.

Na Mwandishi wetu, Uvinza

Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. Mwalikishi wa shirika hilo ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii Bi Rose Haji Mwalimu aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Redio Jamii cha Uvinza FM kilichozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya.

Bi Haji alisema kwamba jitihada hizo ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi wanaishi vijijini ambako hawapati fursa ya kupata habari kwa wepesi kwa ajili ya maendeleo yao kwa sababu wanaishi katika sehemu ambazo hazifikiki kwa urahisi kutokana ya miundombinu duni ya mawasiliano.

"Takwimu zinaonyesha kwamba nchini Tanzania watu wenye uwezo wa kuangalia telelvisheni ni asilimia 7 tu, kwa hiyo redio bado inachukua nafasi kubwa zaidi ya upatikanaji wa taarifa kwa haraka, wepesi, urahisi na kwa mapana zaidi," alisema Bi. Rose Haji. UNESCO ni shirika la Umoja wa Mataifa ambalo kwa muda mrefu limekuwa likitoa msaada kwa redio jamii Tanzania katika kuzianzisha, kuzipatia vifaa na kuzijengea uwezo kiufundi na mafunzo ili zijiendeshe zenyewe.

Redio zilizoanzishwa na UNESCO ziko chini ya mtandao maalum ujulikanao kama Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA).

DSC_0285
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akifanyiwa mahojiano mafupi ndani ya studio za redio jamii Uvinza FM na Mtangazaji wa kituo hicho, Kadisilaus Simon mara baada ya kuzindua rasmi redio hiyo.

Mtandao huo, hutekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuharakisha maendeleo ya wananchi na ushirikishwaji wa wananchi kupitia redio jamii hususan matumizi ya Tehama, mchakato wa Rasimu ya Katiba, uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Takribani Redio za Jamii zipatazo 30, ikiwemo ya Uvinza zinatekeleza mradi maalum wa Uchaguzi unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la (UNDP) kwa kushirikiana na UNESCO, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bara na Unguja (NEC na ZEC) na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP).

"Redio zipatazo 30 zimeshapatiwa mafunzo yanayohusu maadili ya vyombo vya habari, jinsia, na masuala ya jinsi ya kuandika habari za migogoro kwa mtazamo chanya.
Viongozi wa serikali za mitaa pia watashiriki katika mradi huu kuhakikisha uhalali wa mradi huo, wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na makundi maalum pia katika kuhakikisha mwendelezo wa utamaduni wa kuvumiliana, kujadiliana bila kugombana ili kuwezesha uchaguzi mkuu ujao ufanyike kwa amani na utulivu.

"Nina uhakika kuwa ushirikiano huu utaendelea baada ya mafunzo haya na kwamba redio jamii zitaleta mabadiliko makubwa kuhakikisha kuwa migogoro haina nafasi katika jamii zetu. Vyombo vya habari vina wajibu wa kuhakikisha kuwa vinaelimisha jamii juu ya athari za migogoro na kuhamasisha utulivu, amani na uvumilivu katika jamii, " alisema Bi. Rose Haji Mwalimu. Wakati huo huo mwakilishi huyo wa UNESCO Bi Mwalimu ameuomba uongozi wa halmashauri na wanajamii wa Uvinza kushirikiana na Redio Jamii Uvinza FM katika mradi huu ambao utawanufaisha sana wanajamii wa Uvinza na Kigoma kwa ujumla katika kuharakisha maendeleo.

DSC_0308
Mtangazaji wa kituo cha redio jamii Uvinza FM, Kadisilaus Simon akitekeleza majukumu yake kwa furaha kabisa mara baada ya kupewa baraka na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya.

at Tuesday, October 07, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

3
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia), akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.(katikati), Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi, na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu.

Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania kupitia huduma ya DSTV imewataka wasanii kupeleka kazi zao ili waweze kutambulika nje na ndani ya nchi. Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Furaha Samalu wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba .

Alisema kifurushi hicho mahususi kwa watanzania chenye chanieli zaidi ya 65 za kitaifa na kimataifa zikiwemo za Maisha Magic Swahili inayoonesha filamu za Kiswahili, chaneli ya telemundo, chaneli ya nickelodeoni na Disney junior zinazoonesha vipindi vya watoto.
Alitaja chaneli nyingine zitakazopatikana kwenye kifurushi hicho ni Afrika magic Epic Movie, Discovery world, CBS Action, CBS reality na CBS drama pamoja na Select sport 1 na 2 kwa vipindi vya michezo.

1
Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Octoba 1,2014 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.

"Uzinduzi wa kifurushi hichi ni jambo la furaha na msisimko sana kwetu kuona kuwa sasawatanzania wanaweza kupata kifurushi kinachokidhi mahitaji yao. "Kila wakati multichoice inafanya jitihada za kudumu namna ya kuwapa wateja wetu uwanja mpana wa burudani kwa uwepo wa filamu , makala, habari, vipindi vya watoto, muziki, vipindi vya dini na michezo," alisema.

Aliongeza kuwa kifurushi hicho kitagharimu kiasi cha shilingi 17,000 kwa mwezi ambapo watakao jiunga watapata DSTV ikiwemo na gharama ya ufundi kwa shilingi 99,000 kwa kipindi maalum.

Alifafanua kuwa kifurushi hicho pia kitawapa fursa watanzania kuangalia Chaneli za Super Sport select1 na 2 ambayo inatonesha ligi kuu ya Uingereza, kombe la klabu bingwa ulaya, ligi kuu ya Hispania, ligi kuu ya Ujerumani pamoja na riadha na ngumi.

2
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kuhusiana na kifurushi hicho.

5
Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
4 br style="background-color: white; font-family: arial, sans-serif; font-size: 13px;" />

at Friday, October 03, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Untitled

Shirika linalojibidisha na kutetea na kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Under the Same Sun, (UTSS) limeteuliwa kushindania Tuzo ya Haki za Binadamu ijulikanayo kama "Tulip" itolewayo nchini Uholanzi. 

Iwapo UTSS watashinda tuzo hiyo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa katika uboreshaji wa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 

Shiriki kwa kupiga kura ili UTSS washinde Tuzo hii na kulinda ndugu zetu wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania kwa kupiga kura hapa chini na kusambambaza tarifa hizi kwa taasisi na watu mbalimbali. Kwa kupiga kura hiyo bofya hapa
 

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Rufaro Chatora (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa kuboresha ushirikiano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Shirika la Umoja wa Mataifa nchini UN lakutana na wanahabari kujadiliana na kudumisha ushirikiano wao katika habari ambapo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wamekuna na viongozi mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ili kujadili kwa pamoja.
UN wameeleza kazi zinazofanywa na shirika hilo ili waweze kushirikiana kwenye mambo mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, elimu na kuzifahamu kazi za mashirika hayo hapa nchini.

Hivyo waandishi na wahariri wa habari wameombwa kudumisha ushirikiano katika kazi zote zinazofanywa na mashirika yanayosaidia nchini kwa kiasi kikubwa. Pia wameweza kuzungumzia ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka kwa kasi sana hivyo kuwataka kuweza kuandika habari zinazowajuza jamii ili kuweza kuuepuka.

Nia na madhumuni ya mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari ni kuweza kujenga ushirikiano madhubuti baina yao na kuweza kushirikiana kwa karibu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wahiriri wa vyombo vya habari nchini ambapo alielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ikiwemo utekelezaji wa agenda mbalimbali za malengo ya milenia.
Bwana Clioni akiendesha mjadala baina ya viongozi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akitoa salamu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati wa mkutano wa kuendeleza ushirkiano baina ya Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari nchini.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akitoa shukrani kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati walipokutana na wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuboresha ushirikiano na mahusiano baina yao.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha mkutano huo baina ya Umoja wa Mataifa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kuboresha mahusiano baina yao na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Untitled
Mkutano ukiendelea huku wengine wakipitia makabrasha mbalimbali yenye taarifa za Umoja wa Mataifa.
Mmoja wa wahariri akihoji swali kwa viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa wakati wa mkutano huo.
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuboresha mahusiano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mashirika ya umoja wa mataifa nchini.