MJEMA BLOG

JICHO LA MWANDISHI

  • RSS
  • Delicious
  • Digg
  • Facebook
  • Twitter
at Friday, November 22, 2013 Posted by Daniel Mjema 0 CommentsNa Mwandishi wetu.


Kijana Ayubu Mnazi Alphonce(24)ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kujikata uume wake kwa kitu alichodai kuwa ni wembe mpya,sababu za kufanya hivyo Ayubu alieleza kuwa inatokana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa ana uhusiano nao wa kimapenzi.


MKASA KAMILI:Ayubu ambaye kwasasa amelazwa wadi namba moja katika hospitali hiyo,imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye jina halijafahamika aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na baadae sehemu ya uume huo alikwenda kuutupa kwenye majani na kurudi chumbani kwake.


Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba  mzazi wa Ayubu baada ya kubaini mtoto wake kuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu akaamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo akagundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.


Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za msingi

ASEMA NI MCHEZO MCHAFU WA KISIASA

Mbunge wa Urambo Magharibi mkoani Tabora, Profesa Juma Kapuya amejitokeza hadharani na kukanusha vikali taarifa za kumbaka mtoto Yatima. Soma taarifa yake kwa wanahabari hapa chini.

Ndugu wanahabari,
Baada ya kumshukuru na kumtukuza mwenyezi Mungu mwingi wa rehema. Natanguliza salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu mwanazuoni na mwanaharakati mwenzangu Dkt Sengondo Mvungi aliyetangulia mbele ya Haki siku chache zilizopita huko Afrika ya kusini.
Ndugu zangu wanahabari,
Wengi mnanifahamu na kuifahamu vema historia yangu katika utendaji kazi na utumishi wa umma wa Watanzania. Nimekuwa nikiitumikia nchi yangu kwa kipindi kirefu katika Nyanja na sekta mbali mbali kuanzia Darasani mpaka kwenye siasa.
Kwa msingi huo, mimi Profesa Juma Kapuya, siku zote ninajikuta mwenye wajibu endelevu wa kuendelea kulitumikia Taifa langu kila siku mpaka kufikia mwisho wa Nguvu zangu.
Ndugu wanahabari,
Hivi karibuni nikiwa huku jimboni kuendelea na shuhuli za utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kumezuka Tuhuma kadhaa zilizoelekezwa dhidi yamgu zikiasisiwa na wanasiasa wenzangu wa ndani na nje ya chama changu ili kudhoofisha juhudi na utendaji wangu wa kila siku.
Tuhuma hizo zisizokuwa na kichwa wala miguu na pia kutokuwa na ukweli wowote, wamekuwa wakizitoa kwa kumtumia msichana anayedai amefanyiwa vitendo visivyofaa na mimi. Mimi simfahamu na sijui hizi shutuma zinatokea wapi.
Ndugu wanahabari,

Kwa tamko hili ninapenda kuwaambia kuwa nimefedheheshwa sana na uwezo mdogo wa kisiasa unaofanywa na hawa watu kwa kuwa dhamira yao haitatimia. Napenda niwakumbushe ndugu zangu kwamba tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na wapinzani wangu wameanza kunichafua ili nionekane sifai.
Ninapenda kuwaambia watanzania na wananchi wa jimbo langu kuwa wanatakiwa wazipuuze taarifa hizi kwa kuwa hazina ukweli wowote na kwamba ni za kutungwa zenye lengo la kunidharirisha na kuniondolea heshima yangu niliyojijengea kwenye jamii kwa kipindi kirefu sasa. Waswahili wanasema dawa ya mjinga ni kumpuuza
Na hili linajidhihirisha zaidi kwa habari hii kuandikwa na chombo kimoja tu cha habari kinachotumiwa na chama kimoja cha siasa na baadhi ya wanasiasa wa chama changu wasiokitakia heri chama chetu, naomba kuwashukuru na kuwapongeza vyombo vingine vya habari kwa umakini wenu wa kuwa na nauelewa wa kutoandika kitu bila kukifanyia uchunguzi na kubaini ukweli ulivyo.

Chombo hiki cha habari kiliwahi kuripoti mwaka jana kuwa kuna mitambo imeingizwa nchini inayoweza kuandika ujumbe na kisha kuufanya uonekane umetoka kwenye namba Fulani, kwa kipindi kile sikuwaelewa, lakini sasa ninawaelewa na nimewaona kuwa wako sahihi na wao ndio waliouingiza mtambo huu na sasa wameamua kuutumia dhidi yangu kwa kutengeneza meseji na kuzihusianisha na mimi. Ninaamini ukweli utawaumbua muda si mrefu.
Ndugu wanahabari,
Nimeijenga heshima yangu na familia yangu kwa jamii yangu kwa kipindi kirefu mno, kwa hivyo siwezi kuruhusu heshima niliyoijenga kwa miongo kadhaa karibiwa na kupotezwa na watu wachache tena kwa muda mfupi namna hii.
Hivyop basi nimechukua hatua za kisheria kuhakikisha heshima yangu inaendelea kulindwa na utu wangu unaheshimiwa.
Nimemwagiza mwanasheria wangu afungue kesi na tayari amewashitaki watu wote wanaohusika kwenye mpango huu na tayari wameshapokea taarifa ya kuitwa mahakamani.
Nitaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaoendelea kutaka kujipatia umaarufu ama wa kisiasa au wowote ule kwa kutumia jina langu.
Hayo yote ni kwa kuzingatia ukweli kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya kisheria na kufuata na kuheshimu haki na wajibu wakila mmoja wetu.
Kwenye hilo ninawaambia ‘’janja yao nimeigundua, na hawatafanikiwa’’
Ninatoa Rai kwa yeyote mwenye kuona hilo jambo lina ukweli alipeleke kwenye vyombo husika ili lishuhulikiwe kwa mujibu wa sheria na sio kutumia vyombo vya habari kuchafuana.
Mwisho ninasisitiza kuwa nitaendelea kuilinda na kuitetea heshima yangu niliyojijengea kwa jamii kwa muda mrefu sasa na sitaruhusukuiona ikiharibiwa na wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi.
Tuendelee kuijenga nchi yetu,
Mungu Ibariki Tanzania

Imetolewa leo tarehe 15.11.2013 nami
Prof. Juma A.Kapuya
Mbunge – urambo magharibi
S.L.P 45 Kaliua Tabora
Simu 0784993930ALIYEKUWA AKITOA MIMBA NA ANAYETOLEWA WOTE WABURUZWA MAHAKAMANI

Ripota Wetu,Moshi

Daktari mstaafu wa hospitali ya Serikali ya mkoa Kilimanjaro ya Mawenzi, Dk. Francis Shayo (56)amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumtoa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19.

Mwanafunzi huyo wa shule ya sekondari ya Komkwa Masama wilayani Hai, Irene Massawe naye ameunganishwa katika kesi hiyo namba 528/2013 iliyofunguliwa jana akiwa mshitakiwa wa tatu.

Washitakiwa wote watano walifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wilaya ya Moshi, Ruth Mkisi na kupekwa rumande gereza la Karanga mjini Moshi baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni Dk. Shayo na wa pili akiwa ni Peter Mwanga (50) ambaye  anatuhumiwa kushiriki katika njama na mipango ya utoaji mimba hiyo ya mwanafunzi.

Kulingana na hati ya mashitaka,mshitakiwa wa tatu ni Irene, wanne ni Beatrice Urassa (36) na Rose Uronu (38) ambao kwa pamoja ukimuondoa Dk. Shayo wanatuhumiwa kula njama kutenda kosa hilo.

Wakili wa Serikali , Nasir Kassim anayeendesha kesi hiyo, alidai katika siku, tarehe na saa isiyojulikana washitakiwa wote watano walikula njama ya kutenda kosa la kutoa mimba kinyume cha sheria.

Katika shitaka la Pili linalomhusu Dk. Shayo pekee, wakili Kassim alidai Novemba 5 mwaka huu, mshitakiwa alijaribu kumtoa mimba mwanafunzi huyo kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Shitaka la tatu linamhusu Irene pekee ambaye anashitakiwa na Jamhuri kwa kutoka kutoa mimba hiyo huku akifahamu kuwa kwa kufanya hivyo ni kosa la jinai chini ya kanuni ya adhabu.

Washitakiwa wote wamekanusha mashitaka hayo ambapo wakili Kassim alisema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika ambapo Hakimu Mkisi alipanga Novemba 26 kama siku ya usikilizwaji wa awali.

Kwa picha za namna walivyokamatwa rejea picha zilizotangulia.


at Saturday, November 16, 2013 Posted by Daniel Mjema 0 Comments Washitakiwa kwa unyang'anyi wa kutumia silaha

Ripota Wetu,Moshi

Watu wawili wanaotuhumiwa kumteka nyara mwanamke wa Moshi,Asha Amin na kumpora Dola 11,000 za Marekani sawa na Sh18 milioni wamefikishwa kortini kwa unyang’anyi wa kutumia silaha.

Mshitakiwa wa kwanza Deo Mugassa
Wakati watuhumiwa hao wakifikishwa mahakamani juzi, Jeshi la Polisi limesema bado linawasaka watuhumiwa wengine wawili akiwamo kiongozi mmoja wa kisiasa kuhusiana na tukio hilo.

Waliofikishwa mbele ya Hakimu mkazi mkoa Kilimanjaro, Theotimus Swai ni Deo Mugasa (38) mkazi wa Jijini Dar Es Salaam na Gasper Urassa (37) mkazi wa mji wa Bomang’ombe wilayani Hai.

Akiwasomea mashitaka,wakili wa Serikali, Patrick Mwita alidai mahakamani katika siku na sehemu isiyojulikana, watuhumiwa walikula njama ya kutenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa Oktoba 11,2013 huko Soweto NHC mjini Moshi, watuhumiwa walimpora Asha Amin Dola 11,000 (Sh18 mili) baada ya kumtishia kwa silaha aina ya bastola.

Watuhumiwa walikana mashitaka hayo na wamerejeshwa rumande hadi Novemba 27 kesi yao itakapotajwa tena kwa kuwa mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha hayana dhamana kisheria.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi wanaendelea kuwasaka watu wengine (majina yamehifadhiwa) kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo.

Mwanamke huyo alichukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa upelelezi kutoka Jijini Dar Es Salaam wakidai  wametumwa kumkamata kwa tuhuma za kuuza dawa za kulevya.

Kamanda Boaz alisema watu hao walimwachia huru mwanamke huyo siku hiyo hiyo saa 4:00 usiku katika eneo la Bunju Jijini Dar Es Salaam bila kumdhuru na kumpa Sh50,000 za nauli.

Mwili wa mwanamke ukiwa chini ya gari aina ya Fuso muda mfupi baada ya Kugongwa.

Mashuhuda wa Ajali.Mwili wa Marehemu ukiwa umefunikwa.

Baada ya saa moja tangu kutokea ajali gari la kuinua vitu vizito (Winchi)toka Kanan transport lilifika.

Whinchi likiinua gari aina ya Fuso kwa ajili ya kuutoa mwili wa marehemu.

Mwili wa Marehemu ukiwa umetolewa chini ya gari.

Moja kati ya pikipiki mbili zilizogongwa katika eneo hilo kama inayoonekana ikiwa imeharibika vibaya.Moshi.

MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Severina Anthony mkazi wa KCMC amefariki dunia papo hapo baada kugongwa na gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 209 AHA ambalo liliacha njia kisha kugonga pikipiki mbili na kujeruhi watu wengine wawili.


Tukio hilo limetokea jana majira saa 12:15  katika mtaa wa Market jirani kabisa na mgahawa wa Fresh Coach huku mwili wa marehemu huyo ikishuhudiwa ukiwa umegandamizwa chini ya gari hilo kwa takribani saa 1 kutokana na kukosekana kwa vifaa vya uokoaji.


Kwa mujibu wa mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Robert Moshi Limwagu ameiambia clouds fm kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka katika shughuli za kibiashara katika moja ya soko lililopo mjini  Moshi na kwamba mauti ya limfika muda mchache baada ya kufika kumsalimia rafiki yake ambaye anafanya biashara katika eneo hilo.

 

Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wameonekana kusikitishwa na hali ya kukosekana kwa msaada wa haraka hususani gari maalumu la kunyanyulia magari maarufu kama Breack Down hali iliyosababisha marehemu kukaa katika eneo hilo kwa zaidi ya saa 1.
 

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akiwataja wengine walijeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Evarist Kavishe na Cantona Joseph ambao wote wamelazwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC wakipatiwa matibabu.

Boaz amesema chanzo cha ajaili hiyo ni uzembe wa dereva Emanuel Kimari ambaye anadaiwa kuendesha gari akiwa amelewa na kwamba tayari jeshi hilo linamshikilia kwa hojiano zaidi.

 
Mwisho.Afunguliwa kesi mpya ya Ujangili Arusha .

Na Ripota  Wetu,Arusha na Moshi.

Raia wa Pakistani,Kamran Ahmed ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya utoroshaji wa Twiga wanne kwenda Uarabuni kinyume cha sheria, anaonekana kuitesa Serikali ya Tanzania.

Mwezi uliopita, Raia huyo wa Pakistani alifunguliwa mashitaka mapya ya ujangili katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar Es Salaa lakini mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) akayafuta na kuifungua upya.

Hata hivyo upande wa mashitaka umemfungulia mashitaka yanayofanana na hayo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Arusha yakiwemo ya kusafirisha ndege 80 kwenda Guangzhou nchini China.

Wiki mbili zilizopita, wakili wake, Edmund Ngemela alilalamika mahakamani mjini Moshi kuwa upande wa mashitaka hauna nia nzuri na mteja wake kwa kumfungulia mashitaka hayo mapya Jijini Arusha.

Raia huyo wa Pakistan ndiye ambaye anakabiliwa pia na kesi nyingine ya uhujumu Uchumi mjini Moshi ya kusafirisha Wanyamapori hai wakiwamo Twiga wanne kwenda Doha nchini Qatar. Baada ya kufutiwa mashitaka hayo, Jumanne alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 27 na kusomewa mashitaka mawili mbele ya Hakimu mkazi wa mjini Arusha, Devotha Msofe.

Katika shitaka la kwanza, inadaiwa kati ya Januari moja,2005 na Septemba 14,2013 kati ya Dar Es Salaam na Arusha, Kamran alisafirisha nyara za Serikali kwenda Jiji la Guangzhou nchini China.

Ilidaiwa na mawakili wa Serikali Elisaria Zakaria na Agustino Kombe katika kipindi hicho mshitakiwa alisafirisha kwenda China ndege 80 aina ya Pelican wenye thamani ya Dola 4,000 za Marekani. Fedha hizo ni sawa Sh6.4 milioni za Tanzania na kwamba kosa hilo ni kinyume cha kifungu namba 84(1) cha sheria namba 5 ya uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 2009.

Pia ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho hicho katika mikoa ya Dar Es salaam na Arusha, mshitakiwa aliwinda na kuua aina saba ya Wanyamapori wenye thamani ya Dola 28,520 za Marekani. Wanyama hao na thamani yake kwenye mabano ni Tembo (Dola 15,000), Chui (Dola 3,500), Duma (Dola 4,900),Nyati (Dola1,900), Pofu (Dola 1,700), Pundamilia (Dola 1,200) na Swala (Dola 320).

Mshitakiwa huyo alikanusha mashitaka hayo na kuiomba mahakama kumpa dhamana lakini Hakimu akamtaka awasilishe ombi hilo Mahakama Kuu kwani ndiyo yenye uwezo kusikiliza ombi hilo. Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Leo Novemba 12 Jijini Arusha.

at Monday, November 11, 2013 Posted by Daniel Mjema 0 Comments


Mwanga.
Miradi yadaiwa kuhujumiwa . Lengo kupunguza umaarufu wa Profesa Maghembe Ripota Wetu,Mwanga Mgawanyiko mkubwa wa kisiasa unazidi kuitafuna wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro na kutishia kurudisha nyuma shughuli za maendeleo huku baadhi ya miradi ikidaiwa kuhujumiwa.

Uchunguzi umebaini watumishi wa umma, wanasiasa na wananchi wamegawanyika makundi mawili huku kundi moja likimuunga mkono mbunge wa Jimbo hilo,Profesa Jumanne Maghembe.

Inadaiwa baadhi ya watumishi wa umma wanaomuunga mkono mmoja wa wanasiasa wanaotamani Ubunge wa Jimbo hilo akiungwa mkono pia na baadhi ya wazee wanaoheshimika Jimboni humo, wananyooshewa vidole kuwa wanakwamisha miradi ya maendeleo jimboni humo.

“Wanaona kama watasimamia kikamilifu hiyo miradi basi itampa chart (sifa) Profesa Maghembe katika uchaguzi wa 2015 kwa hiyo kuna kusita sita katika kuisimamia”kimedokeza chanzo chetu.

Habari zinadai baadhi ya wafuasi wa kundi linalopinga Profesa Maghembe asipate umaarufu kuelekea uchaguzi wa 2015 ndio waliohujumu mradi wa maji uliopo Kijiji cha Kisangara. Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Shaibu Ndemanga alithibitisha kuhujumiwa kwa mradi huo baada ya watu wasiojulikana kuweka vyuma ndani ya mabomba ya kisima ili mradi usiendelee.

“Siwezi kusema moja kwa moja kwamba uharibifu huo una uhusiano na mgawanyiko wa kisiasa hizo ni hisia tu lakini tumeshatoa hivyo vyuma na mradi unaendelea”alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ipo haja ya wazee mashuhuri wa wilaya hiyo kuangalia uwezekano wa kuyakutanisha makundi yanayohasimiana kwa mustakabali wa baadae wa wilaya hiyo.

Hivi karibuni Profesa Maghembe alikaririwa akisema wapo watu ndani ya wilaya ya Mwanga wanaopinga mradi mkubwa wa maji utakaogharimu zaidi ya Sh56 bilioni kwa sababu tu wanaona utampandisha ‘chati’ yeye kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.

“Wapo watu hapa Mwanga wanapinga mradi huu kwa sababu tu kwa fikra zao utampa chart Maghembe …Tutafute utawala kwa kuleta maendeleo kwa wananchi na si kuharibu mipango mizuri ya kuwaondolea kero wananchi”alisema Profesa Maghembe.

Profesa Maghembe alisema pamoja na mradi huo kunufaisha baadhi ya vijiji vya wilaya ya Mwanga lakini wapo watendaji wachache ambao hawauchukulii kwa uzito unaostahili.