MJEMA BLOG

JICHO LA MWANDISHI

  • RSS
  • Delicious
  • Digg
  • Facebook
  • TwitterNa Dixon Busagaga,Moshi.
POLISI mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kunasa mtandao wa watu wanaodaiwa kujihusisha katika matukio mbalimbali ya unyang’anyi na uporaji wa kutumia silaha za moto ya hivi karibuni baada ya kumkamata mtuhumiwa mwingine na kufanya idadi yao kufikia watano sasa. 


Mbali na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo pia polisi wamefanikiwa kukamata bastola aina ya Browning yenye namba 0663 TZ CAR 75516 pamoja na risasi moja ya bastolailiyotambuliwa kuwa ni mali ya Evance Masuki(54)mkazi wa Majengo mjini Moshi iliyoporwa na watuhumiwa hao October 12 mwaka huu. 


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robrty Boaz alisema katika uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa ,watu hao walikubalia kuonyesha silaha hizo pamoja na risasi tatu za Shortgun ambayo inadaiwa kuhusika katika mauaji ya mfanyabiashara wa mbao mjini hapa Nickson Mushi. 


“Katika hatua za uchunguzi tumebaini kuwepo uhusiano na ushiriki wa silaha aina ya shortgun katika mauaji ya mfanyabiashara Nickson Mushi aliyeuawa huko maili sita Novemba tisa mwaka huu ambayo tunaifanyia uchunguzi wa kitaalamu.”alisema Boaz.


Boaz alisema pia wamefanikiwa kukamata komputa mpakato nyingine aina ya Toshiba ambayo iliibwa hivi karibuni toka kwenye duka liitwalo Pendeza mini super market mali ya William Mwacha mkazi wa mjini Moshi. 


Kamanda Boaz aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na Emanuel Makala(280 maarufu kama Rama,Seif Hussein(42)maarufu kama Mwamba ,Eben Mwaipopo(22)maarufu kama Hashimu,Nicolaus Urio(28) na Emmanuel Kiula(28) wote wakazi wa Moshi. 


Boaz alitoa wito kwa wananchi waendelee kiimarisha vikundi vya ulinzi katika maeneo yao pamoja na kuwa wepesi wa kutoa taarifa za siri za aharifu na uharifu kwa jeshi la polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa mapema kabla ya madahara kutokea. 


Katika siku za karibuni katika mji wa Moshi na mikoa ya jirani kumekuwa na matukio kadha wa kadha ya unyang’anyi na uharifu wa kutumia silaha ambapo miongoni mwa vitu ambavyo vimekuwa vikiporwa ni pamoja na Laptop,Simu pamoja na fedha. 


Juzi kaimu kamanda wa Polisi mkoani hapa, Koika Moita, aliwaambia waandishi wa habari baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi ni pamoja na gari aina ya Toyota Mark II yenye namba T 564 AUW ambalo linaaminika kutumika katika kufanyia uharifu.  


Vitu vingine ambavyo walikutwa navyo watuhumiwa hao mbali na bunduki aina ya Shrtgun pia walikutwa na laptop mbili aina ya Dell na Hp ambazo  taarifa zinasema ziliporwa katika moja ya maduka yaliyopo jengo la Kibo tower mjini hapa. 

Watuhumiwa hao pia walikutwa na vibao vitatu vya namba za gari (Plate number) ambazo ni T916 ARK,vibao viwili na T885 AZW ambavyo vinadaiwa kutumika mara wafanyapo tukio la uharifu kwa lengo la kujificha kunaswa na askari. 


Pia watu hao walikutwa na funguo mbalimbali za magari,Simu nane za aina mbalimbali ,vocha za mitandao mbalimbali ya simu ambazo thamani yake haikuweza kufahamika mara moja pamoja na vifaa mbalimba vinavyoaminika kutumika katika  kuvunjia vikiwemo bisibisi
,Nyundo,Prize  pamoja na Tindo .


Moshi. Shahidi wa 15 wa upande wa mashitaka, Maulid Hamisi, jana aliieleza mahakama namna walivyokamata Wanyampori hai wakiwemo Twiga wanne waliotoroshwa kwenda Uarabuni. Twiga hao na wanyama wengine walitoroshwa kwenda Doha nchini Qartar Novemba 26,2010 kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kwa kutumia ndege kubwa ya Jeshi la Qatar. Shahidi huyo aliiambia mahakama jana chini ya hakimu mkazi mfawidhi,Simon Kobelo kuwa wanyama hao waliwakamata maeneo ya mto wa Mbu,Elboreti na Engaruka wilayani Monduli. Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali mwandamizi, Evetha Mushi, shahidi huyo alidai akiwa na bosi wake ambaye ni mshitakiwa wa kwanza,Kamran Ahmed walikamata Twiga wanne. “Wale Twiga wanne wa mwanzo na Wanyama wengine kama Swala, Pofu na Nyumbu tuliwasafirisha na kuwahifadhi katika zizi la Kamrani lililopo pale Kwarefu (Arusha)”alisema Hamisi. Hata hivyo wakiwa katika hilo zizi Twiga watatu na wanyama wengine nao walikufa ambapo mshitakiwa wa kwanza aliwaelekeza wakakamate Twiga na wanyama wengine ili kujazia waliokufa. Shahidi huyo alisema walirudi tena porini na kukamata Twiga wengine watatu na wanyama wengine na kuwasafirisha hadi kwenye zizi hilo la wanyama wakisubiri kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Alisema Novemba 25,2010 waliagizwa na Kamran kuwaandaa wale wanyama na baadae wakiwa wanaendelea na kazi walikuja watu wanane na kuelezwa kuwa saba kati yao ni marubani wa ndege. Zoezi la kuwaandaa wanyama hao liliendelea hadi saa 9:00 alfajiri ya Novemba 26, ambapo walianza safari kuelekea KIA wakiwa wanafuatana na magari mengine yaliyokuwa yamewabeba wale marubani. Kwa mujibu wa shahidi huyo, baada ya kufikia KIA, milango ilifunguliwa na magari yote manne yakiwemo malori mawili aina ya Mitsubish Fusso yaliyobeba wanyama yaliingia eneo la uwanja. Baadae kazi ya kushusha mabox yaliyokuwa na wanyama ilianza na baadae yalipakizwa katika ndege kubwa ya Jeshi la Qatar ikisimamiwa kwa pamoja na Kamran na marubani wa ndege hiyo ya Jeshi. Alisema wakati kazi ya kupakia wanyama hao ikiendelea, alimuona mshitakiwa wa tatu, Martin Kimath wakijadiliana jambo uwanjani hapo lakini hakuweza kusikia walikuwa wanazungumza nini. Kwa mujibu wa shahidi huyo, baada ya kazi ya kupakia wanyama hao kukamilika, yeye, bosi wake (mshitakiwa wa kwanza) na wafanyakazi wengine walirudi Jijini Arusha kuendelea na kazi nyingine. Alisema baada ya wiki mbili, Kamran aliwaagiza waende tena porini kukamatwa wanyama wakiwemo Twiga ili kujazia wale ambao walisafirishwa na walifanikiwa kukamata Twiga mmoja. “Tulipomfikisha kwenye zizi Yule Twiga alikuwa hawezi kusimama na kesho yake alikufa na hali kama hiyo iliendelea kwa wanyama wengine wadogo hadi zizi likabaki bila wanyama”alisema shahidi huyo. Shahidi huyo alisema mara mbili Twiga hao walipokufa, madaktari kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri) walikuwa wakifika na kuwapasua kisha kuwaelekeza wawazike. Washitakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni pamoja na raia wa Pakistan, Kamran Ahmed, Hawa Mang’unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu ambao wote wako nje kwa dhamana. Wanyama waliotoroshwa kwenda Doha wenye thamani ya Dola 113,715 za Marekani sawa na Sh170.5 milioni za Tanzania, walisafirishwa Novemba 26,2010 kupitia uwanja wa ndege KIA.