MJEMA BLOG

JICHO LA MWANDISHI

  • RSS
  • Delicious
  • Digg
  • Facebook
  • Twitter

Mwathirika wa Saratani ya Ngozi

Wanasayansi wanaamini kuwa unywaji mwingi wa pombe unaweza kuleta hisia zisizo za kawaida mwilini ambazo zinaweza kuiweka ngozi katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya ngozi.

Kemikali ya Ethanol inapogeuzwa kuwa “Acetaldehyde” baada ya ulaji wa chakula,kemikali hii yaweza kuiwezesha ngozi kupenyeza miale hata ya jua (UV light)
Watafiti waliofanya ugunduzi huo, nchini Uingereza wanakubali kwamba kuna mambo mengine yanayochangia mtu kupata Saratani ya Ngozi.

''Utafiti umeonyesha kuwa wagonjwa wanaougua Melanoma huathirika kwa ajili ya kuota jua kwa muda mrefu,hili linaweza kupunguzwa iwapo mtu atajikinga kutokana na jua kali,'' asema Sarah Williams wa Utafiti wa Kansa, Uingereza.

Kulingana na utafiti wao uliochunguza mada 16 tofauti na kushirikisha maelfu ya watu,unywaji wa chupa moja ya pombe moja au zaidi kila siku huongeza uwezekano wa kupata Saratani ya ngozi kwa asilimia ishirini.

Uwezekano wa kupata Saratani uliongezeka sawasawa na unywaji wa pombe,kwa mfano wale waliokunywa gramu 50 ya pombe walikuwa katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya ngozi inayoua watu wengi zaidi duniani ,inayofahamika kama Melanoma.

Daktari Eva Negri,mmoja wa waandishi wa utafiti huu kutoka chuo kikuu cha Milan anasema kuwa unywaji wa pombe unaweza kuathiri uwezo wa mwili kujikinga hasa palipo na mnunurisho Wa miale ya jua. Huu unaweza kuathiri seli kwa kiwango kikubwa na hivyo basi kusababisha Saratani ya ngozi.

Utafiti huu ulinuia kujua ni kwa kiwango gani pombe inachangia kuongeza uwezekano wa kuambukizwa Melanoma,na hivyo basi kuwepo kwa maarifa hii inaweza kuhamasisha watu kujikinga na miale ya jua. Melanoma sanasana hujitokeza kwa mara ya kwa kwanza ngozini kupitia baka jeusi.

Profesa Chris Bunker,rais wa shirika la wataalamu wa ngozi nchini Uingereza alisema kwamba Saratani ya ngozi ndiyo kansa inayoripotiwa zaidi nchini Uingereza na inayowaua watu wengi zaidi nchini humo.Aliongeza kuwa utafiti wowote kwa swala hili unakaribishwa.

Saratani ya Ngozi
Wananchi wa Uingereza hufahamika sana kama wanywaji wa pombe na wenye kupenda kuota jua, hivyo basi utafiti huu utawaruhusu watu kufanya maamuzi bora kuhusu afya zao.

Melanoma

Dalili ya kwanza ya Melanoma ni kuwepo kwa baka jeusi ngozini au kubadilika kwa baka lililokuwa tayari kwenye mwili.Hili laweza kufanyika katika sehemu yoyote mwilini hata hivyo miguu,mikono na uso huathirika pakubwa.

Kwa mara nyingi Melanoma huwa na umbo tofautitofauti na rangi zaidi ya moja.Yaweza kuwa kubwa na mara kwa mara huwasha na kuvuja damu.

''Tunawahimiza watu kujitunza wanapokuwa chini ya miale ya jua .Kwa kuwa watu wengi hupenda kunywa mara kwa mara wanapobarizi, lengo letu ni kuwahamasisha kutahadhari na kukinga ngozi zao kila wakati.''
Mara nyingi baada ya kuota jua wakati wa likizo, wengi hubambuka ngozi.

Mtaalamu Sarah Williams wa shirika la utafiti wa SarataniKansa anasema kuwa uchunguzi huu hauelezi kikamilifu kinachosababisha Melanoma.Hii ni kwa kuwa watafiti wenyewe wanaeleza kuwa, matokeo hayo ni kwa ajili ya miale ya jua wala si pombe. 

Utafiti nao umeonyesha kuwa Melanoma inatokana na kuota jua kwa muda na kubambuka ngozi:unaweza kujikinga kwa kujikinga na jua.Kulingana na uchunguzi wake,jua nchini Uingereza halina nguvu zaidi kusababisha Sarataniy a ngozi, hata hivyo usisahau kukinga ngozi yako unapokwenda kupata jua wakati wa majira ya baridi.

Na kugusia swala la pombe na Saratani ya ngozi, ni muhimu kupunguza kiwango cha pombe unachokunywa. Pombe imetajwa kusababisha aina saba za kansa hivyo basi, Kupunguza unywaji yaweza kupunguza uwezekano wa kuambukizwa Saratani ya ngozi.

Polisi Nchini Tanzania wanamsaka mtu mmoja aliyewauwa watu nane kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine watatu.Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, siku ya Jumamosi usiku eneo la Kaskazini mwa Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Mashuhuda wa tukio hilo, Jambazi hilo lilikuwa likitaka kupewa pesa na simu za mkononi toka kwa waathiriwa.

Kikosi maalum kinachojumuisha maafisa wa polisi wapatao 160 kimeundwa na mekabidhiwa jukumu la kumsaka jambazi huyo kwa nia ya kumtia mbaroni.

Mwanahabari wa BBC Nchini Tanzania anasema kuwa sio kawaida kwa watu wa Mara wanaopakana na Ziwa Victoria kubeba bunduki katika harakati za kulinda mifugo wao.

at Thursday, January 30, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa BBC aliyeaga dunia wiki jana Ann Waithera umechomwa katika eneo la makaburi ya umma la Lang'ata mjini Nairobi.

Ulikuwa wasia wa Ann aliyekuwa anapenda sana kutunza mazingira kuwa mwili wake uchomwe na kisha majivu yake yatupwe kwenye mto na mengine kuwekwa katika eneo ambako kutapandwa mti kama kumbukumbu kwake.
Ann aliyekuwa na umri wa miaka 39 alifariki baada ya kuugua Saratani ya ubongo kwa miaka miwili tangu mwaka 2012.Aliwahi kufanya kazi na mashirika mawili ya habari nchini Kenya, Nation na Citizen kama mtangazaji wa televisheni kabla ya kujiunga na shirika habari la kimataifa la BBC.

Katika BBC, alikuwa anafanya kazi kama ripota wa redio na televisheni hasa alipokwenda Ethiopia, kama ripota wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza.Wakuu wa idhaa ya BBC Swahili David Okwemba, Ali Saleh na mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera wamemtaja Ann kama mchapa kazi na mfanyakazi aliyependa kujituma na kwamba BBC imepoteza mwandishi habari mahiri sana Afrika.

at Thursday, January 30, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni, iliyoko katika Kata ya Ruvu, wilayani Same, alipotembelea kijiji hicho akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, kijiji hicho kimekuwa katika mgogoro wa wakulima na wafugaji kwa zaidi ya miaka 20 sasa tangu mwaka 1987.
Wanakiji katika kijiji cha Ruvu Jiungeni, iliyoko katika Kata ya Ruvu, wilayani Same, wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa mkoa huo, Leonidas Gama wakati alipotembelea kijiji hicho kutatua mgogogro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji

Wanakiji katika kijiji cha Ruvu Jiungeni, iliyoko katika Kata ya Ruvu, wilayani Same, wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa mkoa huo, Leonidas Gama wakati alipotembelea kijiji hicho kutatua mgogogro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni Lepuruka Laize, akifafanua kiini cha mgogoro wa siku nyingi baina ya wakulima na wafugaji katika kijiji, mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Gama akitoa maamuzi ya serikali kuhusu Mgogoro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Ruvu Jiungeni, kata ya Ruvu, wilayani Same, Mgogoroulioanza tangu mwaka 1987.
Mmoja ya wazee wa Jamii ya Wakulima akizungumza mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, iliyotembelea kijiji cha Ruvu Jiungeni, Kata ya Ruvu, wilayani Same, kutoa ufumbuzi wa mgogoro huo.
Wanakijiji jamii ya wafugaji katika kijiji cha Ruvu Jiungeni, Kata ya Ruvu, wilayani Same, wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa mkoa huo, Leonidas Gama wakati alipotembelea kijiji hicho kutatua mgogogro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji

at Thursday, January 30, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma
Viongozi wa Afrika wameanza mkutano wao katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ambapo agenda yao kuu itakuwa swala la mizozo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini.

Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa tume ya Umoja huo Nkosazana-Dlamini Zuma amewaambia viongozi 54 ambao ni wanachama wa Muungano wa Afrika, kwamba wanapaswa kushirikiana ili kuleta suluhu ya kudumu kwa migogoro Afrika.
Jamhuri ya Afrika ya kati imekumbwa na mgogoro wa kisisa kwa miezi kumi sasa tangu waasi kuipindua serikali.Katika taifa jirani ya Sudan Kusini, makundi hasimu yalitia saini ya mapatano juma lililopita baada ya mapigano makali yaliyodumu mwezi mmoja, lakini mapigano yangali yanatokota kati ya serikali na waasi.
Maelfu ya watu wameuwawa katika mzozo huo.

Mkutano huo pia utaangazia,tatizo la uhaba wa chakula na kilimo katika bara hilo. Licha ya uchumi kukuwa katika sehemu nyingi za Afrika,eneo la Sahel na upembe wa Afrika ni maeneo ambayo hukumbwa na tatizo la uhaba wa chakula mara kwa mara. 

Muungano wa Afrika umekosolewa kwa kujikokota katika kuchukua hatua kukabiliana na migogoro ya kisiasa Afrika ya Kati na Sudan Kusini.Muungano huo umemteua Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kama mwenyekiti wake mpya.

Generali Abdel Aziz aliingia mamlakani nchini Mauritania mwaka 2009, baada ya kuongoza matukio mawili ya mapinduzi katika kipindi cha miaka minne.

at Thursday, January 30, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Justin Bieber mashakani
Mwanamziki mashuhuri wa muziki wa 'pop' kutoka Canada Justin Bieber amefunguliwa mashtaka ya kumpiga dereva wa gari la kifahari la kukodisha mwezi Disemba mwaka uliopita.

Bwana Bieber aliye na umri wa miaka 19 alikaribishwa katika katika kituo cha polisi cha Toronto na kikosi kikubwa cha wapiga picha za televisheni pamoja na unyende wa mashabiki wake chipukizi.Amefunguliwa mashtaka chini ya juma moja baada ya kukamatwa mjini Florida marekani kwa shutuma za kuendesha gari akiwa mlevi na mashtaka mengine.

Mwanasheria wa Marekani anayemwakilisha mwimbaji huyo amesema mteja wake hana makosa.

Kwa mujibu wa polisi wa Toronto, yapata saa 02:50 saa za Canada tarehe 30 Disemba, gari la kifahari liliwasili kumchukuwa bwana Bieber na wenzake watano katika kilabu moja ya starehe ili kuwarejesha katika chumba chao cha hoteli.

Na wakati walipokuwa njiani, dereva huyo pamoja na mmoja wa abiria wake, aliyetajwa kama bwana Bieber, wanasemekana kuanza kufokeana maneno makali.Abiria huyo "alimgonga dereva wa limousine hiyo kwenye kisogo mara kadhaa", polisi wamesema.

Dereva huyo anasemekana kusimamisha gari lake na kisha kutoka nje na kuwaita polisi. Mshukiwa 'alichana mbuga' kabla ya polisi kuwasili.Bwana Bieber alijisalimisha kwa polisi Jumatano. Anatarajiwa kufikishwa kizimbani tarehe kumi mwezi Machi.

Justin Bieber amekuwa na 'vituko' katika siku za hivi karibuni


Howard Weitzman, wakili wa Bwana Bieber mjini California, amesema msanii huyo hana hatia na kwamba anatarajia kesi hiyo itachukuliwa kama kosa dogo tu. 

Kuendesha gari akiwa mlevi

Kadhalika siku ya Jumatano, ombi la kutaka bwana Bieber atimuliwe nchini marekani lilipata sahihi laki moja.
Ombi hilo liliwasilishwa kwenye mtandao mmoja wa Ikulu ya White House na raia mmoja wa Marekani.
Rais wa Marekani hana madaraka ya kuamuru mtu kuondolewa kwa lazima nchini Marekani, na haijabainika iwapo Ikulu ya White House itajibu ombi hilo.

Bwana Justin Beiber amejikuta matatani mara kadhaa na maafisa wa polisi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.Mapema asubuhi Alhamisi iliyopita, bwana Bieber alikamatwa kwenye Ufukwe wa Miami baada ya afisa mmoja wa polisi kumfumania akiendesha kwa kasi gari la kukodi aina ya Lamborghini rangi ya njano kwenye barabara ya umma.

Akimshuku kuwa alikuwa mlevi afisa huyo alimtia mbaroni.Kadhalika alifunguliwa mashtaka ya kupinga kukamatwa na pia kuendesha gari akiwa na leseni iliyopita muda wa matumizi.

at Thursday, January 30, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Wabunge wa Ukraine

Na Reporter Wetu, Ukraine

Bunge la Ukraine limeidhinisha sheria inayotoa msamaha kwa waandamanaji waliozuiliwa wakati wa vurugu zilikumba taifa hilo katika siku za hivi karibuni.

Vyama vya upinzani vilisusia kura hiyo kulalamikia kifungu katika mswada wa sheria hiyo ambacho kinasema msamaha utatolewa tu ikiwa waandamanaji watasalimisha majengo ya serikali ambayo wameteka katika siku za hivi karibuni.

Waandamanaji katika baarabara za mji mkuu wa Kiev kadhalika wamekatalia mbali hatua hiyo.

Maandamano hayo yalianza mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya rais Viktor Yanukovych kubatili uamuzi wa kusaini mkataba wa kibiashara kati ya Ukraine na umoja wa ulaya.Kisha baadaye akatia saini mkataba wa mkopo wa takriban dola bilioni 15 na Urusi.
Maandamano bado yanaendelea nchini Ukraine.Hapo jana jumatano, mkuu wa sera za za kigeni katika umoja wa Ulaya Catherini Ashton alisema kuwa amegutushwa na vurugu zilizosababisha maafa katika mji wa mkuu wa Kiev na maneo mengine ya taifa hilo.

" Ni lazima nisema kuwa nimegutushwa sana anasema Bi. Ashton, na ripoti na ripoti ambazo nimepata kuhusu hali ilivyo na bila shaka mojawepo wa maswala muhimu tunayopaswa kushugulikia ni kuzuia vurugu na vitisha. 

Nina wasiwasi kuhusu watu ambao inaonekana wametoweka. Kuna gumzo kali kwamba ukijadili hili na watu wengi, kuhusu watu kuwa katika hali iliyo sawa na mateka na mengine yanayotokana na vurugu ni sharti yakome. Ni swala lenye umuhmu mkubwa,'' anasema Bi Catherine Ashton

Catherine Ashton - ambaye yuko mjini Kiev kufanya mazungumzo na bwana Yanukovych pamoja na makundi ya upinzani amesema Ukraine inahitaji suluhu ya kisiasa itakayopatikana kwa haraka na kumshirikisha kila mmoja.

Hapo jana jioni mswada huo wa kutoa msamaha ulipitishwa kwa kura 232 dhidi ya 11, huku chama cha Bwana Yanukovych cha Party of the Regions kilicho na idadi kubwa ya wabunge kikiunga mkono.
Lakini wabunge 173 hawakupiga huku wabunge wa upinzani wakipiga mayowe kupinga kura hiyo.

Na Reporter Wetu, London

Shirika la habari la BBC limempoteza mwandishi wa habari Ann Waithera. Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiugua Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili.Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia.

Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na Citizen TV. Ann alikuwa na umri wa miaka 39.Waandishi wenza wa Ann BBC wameelezea masikitiko yao na jinsi watakavyomkumbuka Ann katika enzi zake alipokuwa anafanya kazi nao.

Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC amesema : "Nimeshtushwa sana na kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu mpenda watu na mwenye matumaini kwa kila jambo. Mungu ambariki.'' Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kumpoteza Ann.


''Nimehuzinika sana. Anne alikuwa mwandishi mahiri . Kila nilipomtembelea nilivutiwa sana na matumaini ya Ann kupona. Hata katika mkesha wa krismasi, nilipozungumza na Ann alikuwa mcheshi sana. Nakumbuka Ann ndiye alikuwa mwandishi wetu wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha zaidi ya moja mjini Addis Ababa Ethiopia,'' alisema Solomon

Mkuu wa idhaa ya kiswahili ya BBC Ali Saleh naye pia ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Ann akimkumbuka kama mwandishi mahiri na mwenye kujitolea kwa kazi zake.'Nakumbuka kufanya naye kazi kabla ya yeye kwenda Addis Ababa, na kufanya mipango ya kila alichotarajiwa kufanya. Matumaini mengi ila yamekatizwa mapema mno.'' 

alisema Elizabeth Blunt aliyekuwa mwandishi wa BBC mjini Addis Ababa kabla ya Ann kuchukua usukani kutoka kwake. "Anne alikuwa mmoja wa waandishi mahiri wa BBC nchini Kenya . Kifo kimetupokonya mmoja wa waandishi wenye talanta kuu Afrika Mashariki.'' Kauli ya David Okwemba mhariri mkuu wa ofisi ya BBC Nairobi Kenya.

Mhariri mkuu wa idhaa ya Hausa mjini London Mansur Liman, ametuma rambi rambi kwa familia ya Ann, akiwaombea utulivu wakati huu mgumu.

at Tuesday, January 28, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments
Na Reporter Wetu, Nairobi

Mahakama nchini Kenya imemtoza faini ya shilingi milioni 20 au dola laki mbili na thelathini raia mmoja mchina kwa kuhusika na biashara haramu ya pembe za ndovu.Adhabu hii inatokana na sheria kali za kudhibiti uwindaji wa wanyama pori.
Tang Yong Jian alikamatwa wiki jana akiwa na Pembe za Ndovu zenye kilo 3.4 katika sanduku lake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.Ikiwa atashindwa kulipa faini hiyo huenda akafungwa miaka saba gerezani.

Kenya iliharamisha biashara ya pembe za Ndovu mwaka 1989, lakini kumekuwa na ongezeko la biashara hiyo haramu katika miaka ya hivi karibuni.Kuna hitaji kubwa la pembe hizo barani Asia kwa matumizi ya mapambo huku wahifadhi wa mazingira wakishuku kuwa pembe za Vifaru hutumiwa kama dawa Mashariki mwa Bara Asia.

Nchini Kenya kilo moja ya Pembe za Ndovu, inaweza kukugharimu kati ya shilingi 12,000-18,000.

Uwindaji haramu umetajwa kama bishara haramu ya kimataifa ambapo wawindaji hasa huwawinda ndovu na vifaru kwa wingi. Ni hapo jana tu ambapo kifaru mmoja aliyetambulika kwa jina Josephina, aliuawa katika mbuga ya wanyama ya Nairobi.


Kenya inakabiliwa na changamoto ya kuwindwa kiharamu kwa Ndovu zake
Alikuwa kifaru wa kike mwenye umri wa miaka minne. Maafisa wa kulinda wanyama pori wanasema kuwa, kuuawa kwa Joeshina ni mfano mbaya kwani Vifaru wa kike wana umuhimu mkubwa katika kuongeza idadi ya wanyama hao wanapozaana.

Kwa muda wa wiki moja nchini Kenya, kimeripotiwa matukio manne ya uwindaji haramu katika mbuga tofauti tofauti.Mkuu wa shirika la kulinda wanyama pori nchini Kenya, bwana William Kipsang, anasema kuwa tatizo la uwindaji linachangiwa na maswala ambayo hawawezi kudhibiti kama shirika.

''Serikali ya Kenya imetumia mamilioni ya fedha kuhifadhi wanyama pori , lakini nchini Kenya na kwingineko barani Afrika raia wengi wangependa kuona usalama wa binadamu ukishughulikiwa kwanza badala ya wanyama pori. Vile vile watu wengi huishi katika miji iliyo mbali na misitu na wanyama hao,'' alisema Kipsang

Mashirika ya kulinda wanyama wanasema ikiwa tatizo la uwindaji haramu halitatatuliwa, basi kwa muda wa miaka ishirini, ndovu na vifaru barani Afrika hawatokuwepo tena.Asilimia kumi ya uchumi wa Kenya hutegemea utalii, ikiwa Kenya itapoteza Ndovu na vifaru wake, basi sekta ya utalii itaathirika pakubwa.

at Tuesday, January 28, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Utawala bora), Kapten Geroge Mkuchika (wa kwanza), Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama na Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro, Iddi Juma wakiwasili katika kikao cha 30 cha kamati ya ushauri ya Mkoa huo leo.
Mkuu wa wilaya ya Rombo, Dkt. Elinasi Palangyo katika kikao cha leo cha kamati ya ushauri ya mkoa
Wajumbe wa kikao cha 30 cha kamati ya ushauri wa Mkoa wa Kilimanjaro, kilichofanyika leo, katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo, wakimsikiliza Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Utawala bora), Kapten Geroge Mkuchika.
Meneja wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa kilimanjaro, Lawrence Maswa akiwasilisha mada katika kikao cha 30 cha kamati ya ushauri ya mkoa huo leo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama (katikati) katika kikao cha 30 cha kamati ya ushauri ya mkoa huo, uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa, kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa, Iddi Juma na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Dkt. Ibrahim Msengi, kushoto kwake ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Utawala bora), Kapten Geroge Mkuchika na Katibu Tawala Mkoa, Dkt. Faisal Ismail.
Wajumbe wa kikao cha 30 cha kamati ya ushauri wa Mkoa wa Kilimanjaro, kilichofanyika leo, katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo, wakimsikiliza Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Utawala bora), Kapten Geroge Mkuchika.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama katika kikao cha 30 cha kamati ya ushauri ya mkoa huo, uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa, Iddi Juma, kushoto kwake ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Utawala bora), Kapten Geroge Mkuchika.
Mwenyekiti wa TLP na Mbunge wa Vunjo, Dkt. Augustino Lyatonga Mrema, akimsikiliza mgeni rasmi, Waziri wa nchi ofisi ya Rais, (Utawala bora), Kapteni George Mkuchika (hayupo pichani) katika kikao cha 30 cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Kilimanjaro, uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa.

Hii ndio opereshen M4C pamoja daima, chopa inajiandaa kufanya kazi yake, namuona mwandishi wa Nipashe, Godfrey Mushi akituunga mkono.
Dickson Busagaga, Kija Elias na Tundu Lissu wakisaidia kusukuma Choppa
Tundu Lissu akijiweka tayari kuanza safari ya M4C Pamoja Daima katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi, mwishoni mwa wiki iliyopita
Rubani wa Choppa akielekea kwenye sehemu yake baada ya kuhakikisha Tundu Lissu yuko salama kwenye kiti chake kabla ya kuanza safari
Muda wa kuondoka unakaribia Tundu Lissu magazeti utasoma baadae
Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema baada ya kuagana na Tundu Lissu
Choppa linaanza kuruka sasa
Peoples Power tunakuja Tanga kwa kutumia Choppa ya "Babu" Ndesamburo

at Monday, January 27, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Arnold Swai (wa kwanza kushoto)wakati wa upigaji kura, zoezi lilofanyika juzi, wilayani Hai kuziba pengo la nafasi ya Mwenyekiti
Mjumbe wa Halmshauri kuu CCM wilaya ya Hai, Fuya Kimbita, akizungumza katika zoezi la kupiga kura lililoshuhudia Mwandishi wa Habari Leo, Arnold Swai akiibuka kidedea.
Arnold Swai akihutubia baada ya kutangazwa Mwenyekiti Mpya kwa kushinda uchaguzi uliofanyika juzi. Swai alipata kura 151 kati ya kura 222 zilizopigwa
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro, Fredy Mushi, akizungumza na wanajumuiya hiyo muda mfupi kabala ya uchaguzi ulioshuhudia ushindi wa kishindo wa Mwandishi wa Habari Leo, Arnold Swai kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai.

at Monday, January 27, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Wajumbe wa mkutano mkuu wa tatu wa umoja wa machifu Tanzania (UMT) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kufanya mkutano huo, jana katika ukumbi wa kibo Hoetel, iliyoko Marangu, Mkoani Kilimanjaro, waliokaa ni Mwenyekiti wa Umoja huo, Frank Marealle (aliyevaa vazi la kimangi watatu kulia), pamoja na viongozi wengine.
Wajumbe wa mkutano mkuu wakimsikiliza Mwenyekiti wa umoja huo, Frank Marealle (hayupo pichani)
Mkuu wa mkoa wa simiyu, Frank Mabiti (Mtemi  Kishosha) akisikiliza mada katika Mkutano huo
Wajumbe wa mkutano mkuu wa tatu wa umoja wa machifu Tanzania
Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania, Mangi Frank Marealle (katikati), akizungumza na wajumbe wa mkutano huo, kushoto kwake ni kaimu mwenyekiti, chief Fundikira pamoja na viongozi wengine wajuu wa umoja huo.