MJEMA BLOG

JICHO LA MWANDISHI

  • RSS
  • Delicious
  • Digg
  • Facebook
  • Twitter

Kiongozi wa Extra Bongo Ally Choki jukwaani
 Na Mwandishi Wetu, Moshi

WASANII mbalimbali wanatarajia kutoa burudani kesho usiku katika Ukumbi wa Voda House mjini Moshi ikiwa ni mkesha kabla ya kufanyika kwa mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon Jumapili zitakazoanzia katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika.
  
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema jijini Dar es Salaam jana kuwa burudani hiyo ni moja ya hamasa kabla ya kufanyika kwa mbio hizo.
 
 Aliwataja wasani watakaotoa burudani katika siku ya mkesha huo wa Kilimanjaro Marathon kuwa ni Jambo Squad, The Warriors na Extra Bongo.
 
“Kwa mwaka huu tumeona tufanye tofauti kwa kuweka burudani katika siku ya mkesha kabla ya kufanyika Kilimanjaro Marathon,” alisema.


Alisema pia siku ya mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon kutakuwepo na burudani kutoka kwa Joh Makini, Jambo Squad, Wakali Dancers na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma.Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.

at Thursday, February 27, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

NJIA mpya zitakazotumika wakati wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro mwaka huu, (Kilimanjaro Marathon 2014), zimepimwa na kuridhiwa ambapo mabadiliko hayo yameboreshwa ikilinganishwa na njia za zamani.

Kwa mujibu wa waandaji, marekebisho hayo yamelenga kuboresha usalama barabarani na kuondoa msongamano wa magari wakati yanaendelea.

 Njia zilipimwa na kuridhiwa na katibu wa chama cha kimataifa cha mbio ndefu, (AIMS), Hugh Jones akisaidiana na Michael Hughes wa Nairobi Marathon, Ibrahim Hussein wa shirikisho la vyama vya riadha vya kimataifa, (IAAF), pamoja na John Bayo wa Kilimanjaro Marathon Club.

Akitoa maoni yake kuhusu njia hizo mpya Jones, alisema “Njia hizi mpya ni nzuri na za kuvutia. Hapa utaona kuwa baada ya kuanza kwa nusu marathon na kuingia nusu ya pili ya mbio hizi kwa ujumla, washiriki watajikuta wakijitahidi kupanda kilima. 

Hii ni sehemu ngumu yenye kuchosha lakini washiriki watakutana na mashabiki wengi watakaokuwa wakiwashangilia na kuwatia moyo. Wakiachana na mashabiki mbele watakutana na mazingira mazuri yenye mashamba ya kahawa, mandhari ya kijani chenye kuvutia na mandhari nzuri ya mlima Kilimanjaro.”

Aliongeza, "Punde watakapoiacha barabara kuu ya lami, washiriki watalazimika kuvuka bonde, kisha kuendelea na mteremko kwenye msitu wa kuvutia kabla ya kurudi tena kwenye barabara ya lami na kuendelea na mbio hizo kwa kilomita 11.5.

Hatua hii ina mteremko mzuri ambapo safari hii pamoja na kwamba mlima Kilimanjaro utakuwa nyuma ya washiriki lakini mandhari mbele yao bado zitakuwa ni za kuvutia. Wakati wakirudi maeneo ya Moshi Mjini, washiriki watapita chini ya uvuli mzuri wa miti iliyooteshwa kando kando mwa barabara wakati huo watakuwa wakikaribia kumaliza mbio hizo. 

Uwanja wa Ushirika ambapo ndicho kituo cha kumalizia umekuwa ni sehemu ya faraja kubwa kwa wakimbiaji ambao huwa wamechoka sana na wakati watakapokuwa wanavuka mstari wa kumalizia na kugeuka nyuma, kwa mbali macho yao yatakutana na mandhari ya kuvutia ya mlima Kilimanjaro, mandhari ambayo itawakumbusha kuwa ndiyo kielelezo kikubwa cha wao kushiriki mbio hizo”.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers, John Addison, alisema kuwa njia hizo mpya zilizodhibitishwa hivi karibuni zitakuwa maarufu kutokana na njia hizo kupitia kwenye sehemu ya misitu na mashamba ya kuvutia.

Addison ameendelea kusema kuwa njia hizo mpya zitaboresha usalama barabarani wakati wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Machi 2, 2014 na kwamba zitawapa washiriki faraja na uhakika wa kukimbia kwa uhuru na usalama zaidi.
 
Alisema mbio za kilomita 42.2 zinatarajiwa kuanza saa 12.30 asubuhi katika uwanja wa Ushirika, (MUCCoBS), wakati zile za kilomita 21 zinatarajwa kuanza saa 1.00 ya asubuhi kuanzia lango kuu la kuingilia chuo cha Ushirika, (MUCCoBS), ulioko barabara ya Sokoine.

Amesema zile za kilomita 10 zitakazowashirikisha watu wenye ulemavu zinazodhaminiwa na Gapco, zinatarajiwa kuanza saa 12.45 asubuhi uwanja wa Ushirika, ambapo zitawashirikisha wale wenye baiskeli za magurudumu na zile zenye kuendeshwa kwa mikono pekee.
 
Mbio za kujifurahisha za kilomita 5 na ambazo hudhaminiwa na Vodacom, alisema zinatarajiwa kuanza saa 1.45 asubuhi na zitaanzia katika mzunguko wa barabara ulioko karibu na kituo cha YMCA. Mbio zote zinatarajiwa kuishia katika uwanja wa Ushirika, Moshi.

 Mbio hizo zimeratibiwa hapa nchini na kampuni ya Executive Solutions kama waratibu wa ndani kwa ushirikiano na chama cha riadha nchini, ( AT), chama cha riadha mkoani Kilimanjaro, (KAA), pamoja na Kilimanjaro marathon Club.

Aidha mbio hizo zimedhaminiwa na kufadhiliwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement na KK Security,Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, kampuni ya magari ya CMC, Rwandair, FNB Tanzania, UNFPA na maji ya Kilimanjaro.

at Thursday, February 27, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments


Muda si mrefu Diamond Amefunguka haya hapa chini kuhusu wasanii wanasanii wanao tafuta beef za lazima kutoka kwake ...Jisomee


The new Kilimanjaro Marathon route has just been measured and ratified and looks to be an improvement on the previous routes. The new route is no longer an out and back route, it’s a continuous circuit which should help with traffic and congestion issues. 

The route was measured and ratified yesterday by Hugh Jones , Secretary of Association of International Marathons and Distance Races (AIMS) , assisted by Michael Hughes of the Nairobi Marathon , Ibrahim Hussein of IAAF, and John Bayo of the Kilimanjaro Marathon Club. 

Commenting about the new route, Hugh Jones , Secretary of Association of International Marathons and Distance Races (AIMS) said: “It is an astonishingly beautiful course. Right after the half marathon start and entering the second half of the marathon, runners will be probably be concentrating on getting the climbing done. 

This part of the course is testing but there is plenty of crowd support. As spectators thin out the countryside becomes more noticeable and more beautiful. There are coffee plantations, vivid greenery and if you glance upwards spectacular views of Kilimanjaro.” 

He added that “the off-road section comes at the highest point of the course where runners dip down to cross a ravine, then climb up heavily forested slopes to rejoin the tarmac with 11.5km to run. It’s a gentle downward slope nearly all the way and although your back is now turned to the mountain the views remain impressive. 

Re-entering Moshi town runners pass under protective canopy of trees as they approach the stadium. Stadium finish is always uplifting for tired runners. And when you cross the line and turn around, the view of Mount Kilimanjaro reminds you why you came here.”

John Addison, the Managing Director of Wild Frontiers said the new route which was unveiled recently will prove to be popular, and runs through some beautiful forests and farming areas. The new routes are designed to improve traffic flow and give runners more comfort and enjoyment at this year’s race which is scheduled to take place in Moshi on 2nd March, 2014. 

He added that the Full Marathon starts at 6.30 am from the MUCCoBS stadium while the half marathon will start on Sokoine Road outside MUCCOBS gate at 7am and will finish in the stadium. The Gapco Disabled 10km Marathon which has wheelchair and handcycle categories only starts at 6.45 from MUCCoBS. The Vodacom 5km Fun Run will start at 7.45 am at the YMCA roundabout. All events finish at MUCCoBS.

Executive Solutions are local coordinators of the Kilimanjaro Marathon 2014 in conjunction with AT, Kilimanjaro Athletics Association, and Kilimanjaro Marathon Club. The race is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, and KK Security among others, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA and Kilimanjaro Water.

at Wednesday, February 26, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments


1.  The roads from Arusha Roundabout to approximately 10 kilometres out on Taifa Road will be closed from 6:15am to 8:00am. 


2.   Sokoine road from MUCCoBS to KCMC - Kibosho Corner, and from Lema Road to MUCCoBS  through Kilimanjaro Road will be closed from 6.30am to 8.00am.


3. There will be traffic control and restricted access from YMCA – CLOCK TOWER – BOMA RD – ARUSHA ROUNDABOUT – URU RD – MUCCOBS from 7.30am to 8.15am.


4. Note – drivers using these roads after they have been opened to traffic are asked to drive with caution and look out for slower runners who will still be on the route.


5. It us suggested that tour operators collecting climbers from Mweka should do so after 9.00am and use Mweka / Sokoine Rd , as this will be clear of runners by then.


6.  Motorists are advised to avoid Lema Rd / Kilimanjaro Road / Muccobs Main Gate roads if at all possible.


7. Buses are advised not to leave Moshi for Dar before 8:00am. You can leave Moshi for Arusha via Arusha Roundabout though.


ACCESS TO MUCCOBS


1. No vehicle access through main gate before 8.30am. Parking has been arranged at CCP on Sokoine Road.


2. Vehicle access from Uru Road. Parking is only allowed on East and South of the Stadium. No parking North and West of Stadium.


4. Pedestrian access is allowed before 7.00am through North gate only. After 7.00am – South gate only.


6. Vehicles access to stadium: Only vehicles with MARATHON ENTRY / VIP stickers are allowed inside


7. Pedestrians and vehicles may be subject to search.ACCESS TO VODACOM FUN RUN STARTING POINT


Starts at 7.45am. Starting point is close to the YMCA roundabout.


HALF MARATHON


New start point for half marathon only. The half marathon will start on Sokoine Road outside MUCCOBs gate 07h00 and will finish in the stadium. Runners can park at CCP and assemble inside MUCCoBS gate infront of CRDB Bank. 


FULL MARATHON AND DISABLED


The full and the disabled 10km will start at 6.45am in the stadium as usual. All events finish at MUCCoBS.


Mhe. Dk. Fenella Mukangara
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dk. Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo tarehe 2 Machi, 2014 mjini Moshi.

Aggrey Marealle, Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waratibu wa mbio hizo alisema jana kwamba Dr. Mukangara amekubali kuwa mgeni rasmi na atahuduria sherehe ya utoaji zawadi ambapo atatoa zawadi kwa washindi kumi wa mbio defu za kilomita 42 maarufu kama Full Marathon kwa wanaume na wanawake. 

Aggrey Marealle
“Uwepo wa waziri ni ishara ya uungaji mkono tukio hili na ameeleza kufurahishwa kwake na maandalizi ya hali ya juu ya Kilimanjaro Marathon. Dk. Mukangara ameeleza mara kadhaa kwamba serikali inaunga mkono Kilimanjaro Marathon kwa kutambua mchango wake michezo, utalii na uchumi,” alisema Marealle.

Marealle aliongeza kwamba baada ya sherehe ya utoaji zawadi Waziri ataungana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na mpenda michezo Mhe. Leonidas Gama, wawakilishi wa wadhamini na watu wengine mashuhuri kwenye mlo maalum  wa mchana uliodhaminiwa na Kibo Palace Hotel. 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro binafsi na kupitia ofisi yake amekuwa muungaji mkono wa Kilimanjaro Marathon na amekuwa akifurahia kukaribisha maelfu ya watu wanaokuja Moshi kutoka mataifa mbalimbali.

John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema “mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za  nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.
Waandaaji John Addison wa Wild Frontiers, Mwesiga Kyaruzi wa Executive Solutions na Debbie Harrison
Addison aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu.  Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa t-shirts baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za kuvutia kupitia droo.

Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.

Banda la NMB katika mkutano mkuu wa maafisa wa polisi uliofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro katika chuo cha taaluma ya Polisi Moshi (MPA), kuanzia Februari 17 hadi Februari 22. mkutano huo ulidhaminiwa na benki ya NMB.
Meneja wa Benki ya NMb tawi la Nelson Mandela Moshi, pamoja na maafisa wengine wa Benki hiyo kutoka makao makuu wakisikiliza kwa Makini mada zilizokuwa zkiwasilishwa katika mkutano huo.
Maafisa wa NMB katika banda lao katika viwanja vya chuo cha MPA.
banda la NMB
Meneja huduma wateja binafsi wa NMB, Susan Shumo, akipata mawili matatu kutoka kwa baadhi ya maafisa wa benki hiyo na wahudumu katika banda la NMB kwenye mkutano wa Maafisa wakuu wa Jeshi la Polisi lililofanyika mjini Moshi kuanzia Februari 17-22, chini ya udhamini wa NMB.
Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Tom Borghols (wa kwanza kulia), katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki hiyo kutoka Moshi na Makao makuu, baada ya kumaliza kuwasilisha mada katika mkutano mkuu wa maafisa wakuu wa Polisi
Meneja huduma wateja Binafsi, Susan Shumo na Meneja Mauzo, Josephine Kulwa, wote kutoka Makao makuu wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mada ya NMB kutoka kwa Abdulmajid Nsekela, katika mkutano mkuu wa maafisa wakuu wa Polisi nchini

at Saturday, February 22, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Kutoka kushoto, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani, Mubarrak Abdulwakil, Kaimu IGP, Abdulrahman Kaniki, Mkuu wa Polisi Zanzibar, Ali Mussa Ali na DCI.Isaya Mngulu
Maafisa wakuu wa polisi wakishiriki kuimba wimbo wa maadili ya Jeshi hilo.
Kiongozi wa bendi ya MPA, Dogo Vena na kundi lake wakitumbuiza katika hafla ya kufunga mkutano wa makamishna na Maafisa wakuu wa Jeshi hilo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi makao makuu, Advera Senso.
IGPErnest Mangu akihutubia wakati wa kufungwa kwa mkutano huo jana
Katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani, Mubarrak Abdulwakil (katikati), kushoto kwake ni Mkuu wa jeshi hilo, IGP Ernset Mangu na Kaimu wake DIGP.Abdulrahman Kaniki.
Katibu mkuu akihutubia.

Naibu Katibu mkuu NECTA, Dkt. Charles Msonde
MATOKEO ya Kidato cha nne kwa 2013 yametangazwa huku watahiniwa 235,227 wakifaulu mtihani huo ikiwa ni sawa na asilimia 58.25 ya waliofanya mtihani huo. Jumla ya wanafunzi 404,083 walifanya mtihani huo huku waliofaulu kwa daraja la I-III wakiwa wanafunzi 74,324 sawa na asilimia 21.09 ya waliotahiniwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo jijini Dar es Salaam, shule 10 za sekondari zilizofanya vizuri (zilizoongoza) ni pamoja na St. Francis Girls, Marian Boys, Feza Girls, Precious Blood, Canossa, Marian Girls, Abbey, Anwarite Girls, Rosmini na Don Bosco Seminary.

Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari, Kaimu katibu mkuu wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema katika matokeo ya mwaka 2013, shule kumi za sekondari zilizofanya vibaya zaidi ni pamoja na Singisa Sekondari, Sekondari ya Hurui, Sekondari ya Barabarani, Sekondari ya Nandanga, Sekondari ya Vihokoli, Sekondari ya Chongoleani, Sekondari ya Likawage, Sekondari ya Gwandi, Sekondari ya Rungwa na Sekondari ya Uchindile.

Taarifa hiyo ilifafanua zaidi kuwa kati ya watahiniwa 404,083 waliofanya mtihani wasichana waliofaulu ni 106,792 huku idadi ya wavulana waliofaulu ikifikia 128,435. Wavulana waliopata daraja la kwanza (division one) ni 5,030 huku idadi ya wasichana ikiwa ni 2,549. 

Aidha wavulana waliopata daraja la tatu (division three) ni 27,904 na wasichana ni 17,113. Wanafunzi waliopata daraja la nne (division four) ni 126,828, huku idadi ya wasichana wakiwa 62,841 na wavulana 63,987.

Taarifa imefafanuwa kuwa jumla ya wanafunzi 151,187 wamepata sifuri (division ziro), ambapo idadi ya wasichana ni 72,237 na wavulana ni 78,950.  


Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya leo, Februari 20.
Bi. Shembusho akilia kwa uchungu baada ya kudangasnywa na watu wawili, wa kike na wakiume ambao majina yao bado hayajafahamika. watu hao walimpeleka katika Hoteli maarufu mjini moshi, Fresh Coach na kumtapeli shilingi milioni 5.4 ambazo alikuwa ametoka kutoa Benki ya Uchumi ya mjini Moshi.
Askari wa Hoteli hiyo inayodaiwa kutumika kumtapeli mwanamke huyo akimtuliza Mama huyo ambaye alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo.
Akilia kwa Uchungu
Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi
Uchungu wa kutapeliwa hela
Mama akisimulia tukio zima kwa wananchi waliofika katika eneo la tukio baada ya kumsikia akipinga ukunga kuomba msaada.
Msamaria mwema akimsaidia kupanda ngazi za Hoteli hiyo tayari kwa safari ya kuelekea kituo cha Polisi kutoa Taarifa.
Bi. Shembusho akipanda gari la Msamaria Mwema aliyejitolea kumpeleka Polisi kutoa taarifa hizo. (picha zote na Kija Elias wa Mjema blog)

at Thursday, February 20, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.
 
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa. WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
 
WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.Facebook na WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana.

at Thursday, February 20, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Katika ufuo wa bahari ya Ziwa Viktoria kuna biashara inayovuma-dau za uvuvi zilizotengenezwa kwa mbao zimejaa si haba, asubuhi zimejazwa Samaki wa Tilapia.Nyakati za asubuhi na mchana, wavuvi hukusanyika na kupiga foleni kununua Samaki; wengi wao wakiwemo wanawake ambao wanatumainia kupata faida; japo kidogo, katika soko lililo karibu.
Ila, katika sehemu hii ya Kenya, biashara hii haifanywi kwa ubadilishanaji wa pesa kwa Samaki. Malipo ni ubadilishanaji wa ngono kwa Samaki: wanawake wanauza miili yao kwa matumaini kuwa wataeleka nyumbani na Samaki wengi.
Biashara hii inajulikana kama “ubadilishanaji wa ngono kwa samaki” ama, kwa lugha ya kiluo, inajulikana kama “jaboya”. Lucy Odhiambo, 35, anatayarisha ununuzi wake wa mwisho, ambao ataupeleka sokoni; anawapasua samaki na kuwatoa uchafu wa tumboni. Ni mjane, na mama wa watoto tano, anasema kuwa wanawake hapa wanalazimika kufanya wasiyotarajiwa kufanya na jamii.
"Inanilazimu niuuze mwili wangu kwa wavuvi ili nipate samaki kwa sababu sina uwezo wa kujikimu", anaiambia BBC."Kawaida, mimi hulala na wavuvi wawili au watatu kwa juma. Naweza pata magonjwa, ila sina budi kufanya hivyo. Nina watoto ambao nafaa kuwalipia karo. Jaboya ni tendo baya mno. "  
Ugonjwa anaouongelea hapa ni ukimwi ambao umeenea sana katika eneo hili. Ripoti za afya zinadhihirisha kuwa ugonjwa wa Ukinmwi umekithiri katika eneo hili ukiipiku kwa 15% maradufu ile idadi ya wastani ya nchi. Hii inatokana na biashara hii ya “ubadilishanaji wa ngono kwa samaki.Japo polepole, tabia hii inabadilika, huku ikielekea kuisha.

‘Hatutegemei tena wanaume’

Agnes Auma ananipileka ufuoni mwa bahari katika dau analomiliki. Dau hilo linatumiwa na wavuvi ambao amewaajiri kazi, na wanapovua Samaki, yeye ndiye hufanya uuzaji.
Anawalipa wafanyakazi wake na pia gharama za huduma za dau lake, kisha anasalia na hela kadhaa za kujikimu.Mradi unaoendeshwa na shirika la uthamini la eneo hilo linalooitwa Vired unapata msaada kutoka kwa shirika la Marekani la US Peace Corps, na umeweza kuyabadilisha maisha ya wanawake katika eneo hilo.
Tunapiga gumzo wakati dau linazidi kuingia ndani ya ziwa , huku likipita juu ya magugu, na mimea ya baharini, jitihada inayowafanya wavuvi kuloa jasho."Niliona kuwa ningekufa iwapo ningeendelea kuuza mwlili wangu kwa minajili ya kupata samaki-na singeendelea,” Bi. Auma alisema.
“Mradi huu unanisaidia kupata riziki yangu, hivyo basi, si lazima niwategemee wanaume kujikimu. Na, ninapolipia gharama za huduma za dau, nafanya hivyo nafsi yangu ikiwa safi na tulivu.” Tunapofikia sehemu Fulani ndani ya ziwa, wavu unatupwa majini.
Dakika chache baadaye, wavu unatolewa ukiwa umejaa Samaki.Kisha, samaki mkubwa wa kamongo anainuliwa na kutupwa ndani ya dau, huku Bi. Auma akitazama.“Nina furaha kubwa kutokana na jitihada za wavuvi wangu, pia nina furaha kuwa mimi ni mvuvi wa kike ambaye ana bidii na nguvu,” anasema huku akitabasamu.

Leo hii, mradi huu wa Vired, una idadi ya wanawake 19, ila shirika hilo linatumai kuwa idadi hii itaongezeka kadiri muda utakavyoendelea. "Ubadilishanaji wa ngono kwa Samaki ni biashara yenye hatari kwa sababu, kila siku tunagundua kuwa watu wanakufa kutokana na ugonjwa wa Ukimwi,” anasema Dan Abuto wa shirika la Vired.

"Tunahitaji kuwainua wanawake hawa kiuchumi, kinafsi na pia kijinsia ili waweze kupata namna ya kujikimu na kujisimamia. Tuna furaha kuwa mradi huu unavuna matokeo mazuri, na pia wanawake hawa wanadhihirisha bidii na utashi.”

‘Nina aibu’

Ila, hii ni sehemu moja tu ya nchi yangu ambayo “jaboya” ni maarufu. Na hata hapa, kuna wale wavuvi ambao wanafurahia wakilipwa kwa pesa. Lucy Odhiambo: "Nalazimika kulipia samaki kwa kuuza mwili wangu kwa sababu sina namna nyingine ya kujikimu” 
Nakutana na Felix Ochieng, 26, mvuvi ambaye ameoa ila bado anajihusisha na matendo ya ngono nje ya ndoa na wanawake wengine watatu kwa juma, huku akiwapa samaki. Ananiambia kuwa mwanamke atalipia samaki wa shilingi 1000 kwa pesa taslimu ya shilingi 500 ($6; £3.50), huku akitumia mwili wake kujaza akiba ya hiyo shilingi 500 nyingine iliyosalia.
“Niilirithi tabia hii kutoka kwa babangu mwenye alikuwa akifanya vivi hivi," anasema, huku akiapa kuwa anatumia kinga.Namuuliza iwapo ana aibu kutokana na kile anachofanya.
"Ndiyo, nina aibu,” anajibu huku akiangalia upande wa ziwa, “na ni tendo ovu. Ila, kuna matamanio yanayotokana na wanawake." Bado kuna kazi kubwa inayotarajiwa kufanywa ili kuimaliza tabia hii ambayo imekita mizizi katika sehemu kadhaa nchini.
Ila japo kidogo kila siku, idadi ya wanaoshiriki tabia hii inapungua, na wanawake wanaoishi katika maeneo ya ziwa Viktoria wanapata kujua hatari zinazotokana na biashara hii.Kuimaliza biashara hii ya “ubadilishanaji wa ngono kwa samaki” kabisa, tutahitaji kubadilisha fikra na mitazamo yetu, ili kuweza kupata mtazamo mzuri ulio faafu wa jinsia zote.
Na hiyo itakuwa ngumu kufanikisha; kikwazo cha kuweza kufanya biashara ya ubadilishanaji wa samaki kuwezeshwa na pesa pekee.
MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA SHIRIKA LA HABARI UINGEREZA, BBC

Bondia Francis Cheka, pichani.
HIVI karibuni wadau wa mchezo wa masumbwi walifanya mkutano wa kujadili tasnia hiyo inayokabiriwa na changamoto nyingi, hasa kwa kuona kampuni zinavyouchunia mchezo huo.

Ingawa wamekalia pesa lukuki, lakini wadau hao wameendelea kuziba macho na masikio yao, hata pale tunapoona malalamiko ya wadau wa ngumi na mabondia kuwa wanakosa udhamini.

Changamoto hizo ndio sababu inayoufanya mchezo huo ushindwe kupiga hatua kubwa, jambo lililowafanya wadau hao wakutane katika mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.


Waswahili wanasema kupanga ni kuchagua. Kwakuwa wadau hao wameamua kupanga jinsi ya kukabiriana na changamoto hizo, basi ni jambo jema kwao.

Hata hivyo, wadau hao wanakutana kwenye kikao chao wakati wao wenyewe wakati mwingine hawapo makini. Kwa mfano, mwishoni mwa mwaka jana kulikuwa na kadhia kubwa.

Ni pale promota wa mchezo wa masumbwi, Jay Msangi alivyoutia aibu kwa kuandaa pambano la Kimataifa kati ya Francis Cheka na Mmarekani, Phil Williams.

Ingawa pambano hili la Ubingwa wa Dunia lilimalizika kwa Cheka kushinda na kulitangaza Taifa, ila kasumba ni pale promota alivyoshindwa kujipanga katika suala zima la malipo.Awali mpambano huo ulitaka kushindwa kufanyika, hivyo serikali kuingilia kati kunusuru zogo hilo, ambalo hadi mwisho ingekuwa aibu kwa Tanzania nzima.


Si nia yangu kukumbushia kilichotokea mwezi Agosti mwaka jana, ila ni namna gani wadau wa ngumi wote wanapaswa kufanyia kazi majibu ya mkutano wao.Huu ndio ukweli. Wadau hao wakiamua kufanyia kazi yale waliyoamua wenyewe kwa ajili ya kunusuru tasnia hii itakuwa ni jambo la busara kwao na manufaa ya mchezo wa ngumi.

Huu ni wakati wa kufanya jitihada za kuukomboa mchezo wa masumbwi. Kila mtu mwenye malengo na mchezo wa masumbwi anapaswa kuamua kwa dhati kufanya kila analojua kwa ajili ya maendeleo ya ngumi.Mapromota mfano wa Msangi nao wanapaswa kubadilika na kuamua kufanya juhudi kujijengea heshima ili walau waaminike katika kuandaa mapambano makubwa zaidi.

Kinyume cha hapo kasumba hii itaendelea. Mchezo wa masumbwi utazidi kudidimia. Wadau wakubwa wote watakimbilia katika michezo mingine, hasa mpira wa miguu.Matokeo yake ni kuona ngumi inapoteza thamani yake, ingawa kuna vijana wengi wanaoweza kucheza masumbwi kwa ajili ya maisha yao na Tanzania kwa ujumla.

Mabondia wote wenye kiu ya kucheza ngumi watapoteza thamani yao, maana hakuna juhudi za dhati za kuleta ushindani, ukizingatia kuwa juhudi zao ni sifuri.


Hili linapaswa kuangaliwa upya, hasa kwa kuona mkutano wa wadau wa ngumi umekuwa na tija kwa mchezo huo Tanzania, ili kuleta picha na juhudi halisi za kuendeleza ngumi na kuona vijana wengi wanaibuka kwa kasi kushiriki kwenye masumbwi.

at Wednesday, February 19, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Teknolojia mpya ya upasuaji kwa njia ya Darubini katika Hospitali ya KCMC, Teknolojia hiyo inadaiwa kuokoa muda na gharama za upasuaji pamoja na kupunguza vifo.
Madaktari KCMC wakimfanyia mgonjwa upasuaji kwa kutumia Teknolojia mpya Darubini.
Dkt. Kondo Chilonga akiongoza madaktari wenzake kumfanyia mgonjwa upasuaji kwa kutumia teknolojia mpya ya Darubini ambayo inaruhusu upasuaji kufanyika bila ya kuchana ngozi.
Zoezi linaendelea ukimya tafadhali!!! kwa mbali ni mtaalamu wa upasuaji wa Darubini (mzungu) kutoka Uingereza, Dkt. Liam Horgan.
Dkt. Kondo Chilonga akiongoza madaktari wenzake kumfanyia mgonjwa upasuaji kwa kutumia teknolojia mpya ya Darubini ambayo inaruhusu upasuaji kufanyika bila ya kuchana ngozi.
Madaktari wa Upasuaji kutoka kulia, Fadhili Athumani, Zephania Renatus na Bahati Mustapha katika chumba cha Upasuaji KCMC.
Timu ya waandishi wa habari "madaktari feki", kutoka kushoto, Fadhili Athumani (Mtanzania), Safina Sarwatt (Mtanzania), Flora Temba (Majira), Gabriel Chissou ambaye ni Msemaji wa KCMC, Sauda Shimbo (TBC) na Bahati Mustapha (Moshi Fm) baada ya kumaliza kazi katika Theatre.