MJEMA BLOG

JICHO LA MWANDISHI

  • RSS
  • Delicious
  • Digg
  • Facebook
  • Twitter

Baadhi ya taasisi a NGO'S mbalimbali zilihudhuria uzinduzi huo.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi wakisikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa.
Makundi mbalimbali ya watu yalishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani iliyozinduliwa mjini Moshi.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi wakisikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani.
Mwakilishi  mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Rufaro Chatora akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi huo kutoka Asasi mbalimbali mkoani Kilimanjaro.
Mwakilishi wa UNICEF,Sudha Sharma akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Naibu waziri wa Afya,Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika katika sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Mkurugenzi wa huduma za Afya toka wizara ya Afya,Dk Neema Rusibamayile akitoa neno la shukrani mara baada ya Mke wa rais,Mama Salma Kikwete kutoa hotuba yake.
Mke wa rais ,Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo duniani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa chanjo ya matone kwa mtoto Ahmad Saleh kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo duniani.

at Tuesday, April 29, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiuzindua rasmi mnara wa Vodacom kuashiria kuanza kupatikana huduma za kampuni hiyo ya simu nchini katika kijiji cha Bukuba kilichopo Buhigwe mkoani Kigoma. Pembeni yake ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Malcelina Mbehoma na Mwenyekiti wa Halmashauri Abel Kabona. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Charles Gishuli (mwenye koti) akitumia simu yake ya mkononi kutuma fedha kupitia huduma ya M-pesa mara tu baada ya kuzindua huduma za Vodacom katika kijiji cha Bukuba mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Abel Kabona. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli jinsi ambavyo wakazi wa kijiji cha Bukuba Mkoani Kigoma wanavyoweza kupata huduma za Intaneti kupitia mtandao wa Vodacom mara baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuzindua rasmi huduma za Vodacom kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto (mwenye kofia nyekundu) ni Mhandisi wa Vodacom Mkoa wa Kigoma Adam Nyamgali.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiongea na wakazi wa kijiji cha Bukuba na vijiji jirani waliofika kushuhudia uzinduzi wa mnara wa mtandao wa Vodacom kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Wengine kutoka kuhsoto ni Mhandisi wa Vodacom Adam Nyamgali, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Renatus Mkasa na Kaimu Mkurgenzi Mtendaji wa Wilaya Malcelina Mbehoma. Kupatikana kwa huduma za Vodacom kijijini hapo kunatarajiwa kufungua ukurusa mpya wa maendeleo ya kiuchumi an kijamii kijijini hapo.
Mhandisi wa Vodacom Mkoani Kigoma Adam Nyamgali akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma jenereta inayozalisha umeme wa kuendeshea mnara wa mawasiliano wa kampuni hiyo. Mkuu huyo wa Wiayaa aliuzindua mnara huo uliopo kijiji cha Bukuba mwishoni mwa wiki. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Bunge la Katiba limeahirishwa hadi Jumanne ya Agosti  5 mwaka 2014 kuendelea na vikao vya kujadili Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge la Maalum la Katiba limeahirishwa huku sura ya kwanza na sita ikiwa imeshika kasi kiasi cha kuibua mizozo iliyozalisha chuki kwa baadhi ya wajumbe.

Wajumbe wengi walionekana kuvutana huku baadhi yao wakipinga serikali mbili wakitaka tatu na wengine kusema serikali tatu ni mbaya zibaki mbili. Mvutano huo ulisababisha Wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kujitoa.

Akizungumza wakati anaahirishwa Bunge hilo Maalum la Katiba leo mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, alisema kuwa wajumbe watakutana tena Agosti 5, mwaka 2014 kuanzia saa tatu asubuhi.
Alisema kuwa wajumbe wengi wameonyesha kufanya kazi nzuri kuchangia mijadala ya Katiba Mpya, ingawa changamoto zilikuwa nyingi.

“Natangaza kuahirisha Bunge hili nikiamini kuwa tutakutana tena kuendelea na vikao vyetu kwa ajili ya kuitengeneza Katiba Mpya ya Watanzania,” alisema.

Awali wakati anachangia, Mjumbe wa Bunge hilo, ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, alishangazwa na vijana wadogo kudharau kazi za waasisi wa Taifa hili kwa kisingizio cha kutoa hoja ya Katiba Mpya.

at Friday, April 25, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) amemtaka Mkuu wa Polisi wilayani hapa (OCD), Gires Muroto, kuachia ngazi baada ya kuzuia mikutano yake.

Lema alimtaka OCD huyo kujitoa kwenye uongozi wa Jeshi la Polisi na kwenda kufanya kazi ya uenezi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Lema alisema Aprili 22 mwaka huu aliandika barua ya kuomba ulinzi kwenye mikutano yake.

OCD huyo alifuta mikutano ya shughuli za mbunge huyo aliyoiruhusu kwa kigezo kuwa alipokea maombi mengine ya CCM kufanya mkutano eneo alilotaka kufanya mkutano.
Lema alisema Aprili 23 alipokea barua ya OCD ikimzuia kufanya mkutano kwa hoja kwamba kuna tishio la usalama jijini Arusha kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea kwenye baa ya Arusha Night Park, hivyo hawaruhusu mikusanyiko.

“Mimi ni mwakilishi wa wananchi wa Arusha, watu wangu wamepigwa mabomu, nataka nizungumze nao niwatie moyo nazuiwa… wiki ijayo naenda kwenye kikao cha Bunge la Bajeti, nataka niwasikilize wananituma nikawasemee nini sipewi ruhusa, nataka nisikilize kero za wapiga kura wangu OCD ananizuia.

“Hivi tukimaliza hapa kama madereva wanaogopa kuendesha gari kutangaza mkutano, kazi hiyo nitaifanya mwenyewe, huu ni uhuni kwa sababu kuna mikutano ya injili inaendelea, ibada zinafanywa makanisani na misikitini, masoko ambayo ndiyo yenye mikusanyiko mikubwa inaendelea.

“Kumbi za starehe tena za usiku zinafanya kazi kama kawaida, hata hapo palipopigwa bomu watu wanakusanyika, kwanini mkusanyiko wa mbunge na wananchi wake ndiyo unaonekana kuhatarisha usalama?” alihoji Lema.
Alisema sheria ya kinga, haki na madaraka ya Bunge inamruhusu kuzungumza na wananchi wake kwa uhuru, na yeyote atakayejaribu kumzuia atatenda kosa na anapaswa kushitakiwa.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leberatus Sabas, alipotakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo, alijibu kwa mkato: “Tayari tumeshalimaliza suala hilo, tumeruhusu mikutano yake.”
Awali Aprili 17, mwaka huu, Lema alimwandikia barua OCD akiomba kufanya mikutano ya wananchi kwa nafasi yake kama mbunge kwenye kata za Levelosi, Terrat, Daraja Mbili na Moshono kwa tarehe tofauti.

Lema alisema kuwa siku hiyohiyo alipokea barua toka kwa OCD akimruhusu kuendelea na mikutano yake, lakini katika hali isiyo ya kawaida, Aprili 20, akapokea barua nyingine kutoka kwa kiongozi huyo wa polisi akizuia mikutano hiyo kwa maelezo kuwa Aprili 19, mwaka huu CCM nao wamepeleka barua wakiomba kufanya mikutano maeneo hayo jambo wanaloona linaweza kusababisha uvunjivu wa amani.

Lema amjibu JK
Katika hatua nyingine, Lema amemtaka Rais Jakaya Kikwete aelewe kuwa maandamano ya Jiji la Arusha husababishwa na watendaji wa serikali yake kupindisha sheria na kuminya haki za umma, hivyo huwalazimu kuandamana ili kuzidai.

Alisema kuwa hategemei kusifiwa na kiongozi huyo wa nchi katika harakati zake za kupigania haki ya wananchi wake na siku ikitokea anamsifu, itabidi ajitathmini ni wapi amekosea.Lema alisema jambo la kusikitisha ni kuwa wale wanaohusika na uvunjivu huo wa sheria na haki za binadamu ni kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, na wote wamepandishwa vyeo.DC Mwamoto akiweka  sahii kitabu cha maombolezo  leo
Spika Makinda akitoa  mkono wa pore kwa wafiwa
Spika Makinda  kulia akimpa pore waziri Hawa Ghasia
Spika Makinda  akiwapa pore  wafiwa
Spika  wa bunge Anne Makinda akiwa amepiga magoti  kuwapa  pole  wafiwa katika msiba wa aliyekuwa DC wa kalambo Moshi Chang'a leo mjini Iringa
Waombolezaji  wakiwa katika msiba  huo  leo
Spika wa bunge Anne makinda akisaini kitabu cha maombolezo ya DC Chang'a leo
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasiaakisaini kitabu  cha maombolezoo ya  aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Mussa Chang'a leo nyumbani kwake mjini Iringa kabla ya mazishi  yaliyofanyika makaburi ya Mtwivila 
Spika Anne Makinda akiteta  jambo na waziri Hawa Ghasia  leo
Mwanahabari  Eliasa Ally Chang'a( kulia)  ambae ni ndugu na DC Chang'a akiwa na waombolezaji  wengine Msafiri Mtandi kushoto na Said kalinga katikati
Mwenyekiti  wa CCM Kilolo Sety Mwamoto kulia  akiwa na mdau
mfanyabiashara  mkubwa Iringa Pilly MOhamed  akisainia kitabu cha maombolezo
Mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma akisaini kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya kalambo Rukwa marehemu Moshi  Chang'a wanaoshuhudia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kushoto na mkuu wa wilaya ya  Iringa Dr Leticia Warioba katikati ,hapa ni nyumbani kwa marehemu eneo la Kihesa mjini Iringa
RC Mbeya Bw kandoro  akiwapa pore  wafiwa
Mke wa mkuu wa mkoa wa Mbeya akisaini kitambu cha maombolezo ya Dc Chang'a
Mkuu wa mkoa wa Mbeya akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo
Waombolezaji  na ndugu  wakiwa katika viwanja vya maombolezo  leo
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza akitoa  salam za chama
Kiponza akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro  leo
Mbunge Msigwa akiwa na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akitoa  salama zake na za Chadema pamoja na ubani wa TSh 100,000
Vijana  wa  CCM wakiweka mambo  sawa
Wakuu wa  wilaya  mbali mbali nchini  wakiwa  wameubeba mwili wa DC mwenzao Moshi Chang'a leo
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamwoto  kulia akishirikiana na mkuu wa wilaya ya Mwanza  kukunja bendera  iliyotumika kufunika mwili wa DC Chang'a
Kada wa CCM Iringa mjini Frederick Mwakalebela akishiriki msiba  huo
Wakuu wa wilaya na wananchi  Iringa  wakiwa  wamebeba mwili wa Dc Chang'a mjini Iringa leo
Mwili wa DC Chang'a ukipelekwa msikiti wa Mwanchang'a Kihesa
Waombolezaji  wakielekea msikitini  leo
Umati wa wananchi  wakielekea makaburi ya Mtwivila  leo
Msafara  wa kutoka nyumbani kwa DC Chang'a kwenda msikitini
msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya siasa Ikulu Rajab Luhwavi kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kulia  wakati wakielekea kumzika Dc Chang'a leo mjini Iringa .