MJEMA BLOG

JICHO LA MWANDISHI

  • RSS
  • Delicious
  • Digg
  • Facebook
  • Twitter

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwasilisha Bungeni  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2014/2015 mjini Dodoma tarehe 27 Mei 2014
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha (wa kwanza kulia) pamoja na Mke wa Waziri, Mama Dorcas Membe na Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Mohammed Maundi wakifuatilia kwa makini Hotuba ilikuwa ikitolewa na Mhe. Membe (hayupo pichani) Bungeni.
Katibu Mtendajii wa Jumuiya ya Maedneleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena Tax (katikati) akiwa na wageni wengine wakifutilia Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2014/2015
Baadhi ya Wawakilishi kutoka Balozi za nchi mbalimbali zilizopo hapa nchini wakifuatilia Hotuba ya Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mwakilishi kutoka Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Betty Machangu (Mb.) akiwasilisha Hotuba kwa niaba ya Kamati hiyo
Mhe. Membe (kushoto) akiwa na Naibu wake Mhe. Dkt. Mahadhii Juma Maalim (Mb.) wakifuatilia hotuba wakati Mhe. Machangu (hayupo pichani) akiwasilisha
Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje kutoka Kambi ya Upinzani, Mhe. Ezekiel Wenje nae akiwasilisha hotuba ya kambi yake.
Mhe. Membe akiongozana na Mhe. Wenje kutoka Bungeni mara baada ya kipindi cha mchana kumalizika.
Mhe. Membe, Mama Dorcas Membe (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Dkt. Tax  wakiwa nje ya Viwanja vya Bunge mara baada ya kipindi cha mchana kumalizika

 
Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta  akisoma Bungeni hotuba ya Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015. Bajeti hiyo ilijadiliwa na kupitishwa na Bunge. Bajeti hiyo pia ilisikilizwa na Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliokuwepo Bungeni siku hiyo. 
Mbunge Shy-Rose Bhanji (kushoto) akiwa na wabunge wa Bunge la Muungano.
Shy-Rose Bhanji akizungumza na Mbunge Mwenzake wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere. 
Bhanji ndani ya viwanja vya Bunge...
Wabunge wakiwa viwanja vya Bunge...

Picha ya pamoja na baadhi yua Wabunge na mawaziri wa Bunge la Muungano. 
Makongoro Nyerere na Mheshimiwa Wasira.
Picha na Wabunge mbalimbali

at Sunday, May 25, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Eng. Gerson Lwenge akiapishwa. Pichani kutoka. kushoto, Msajili wa Bodi ya Makandarasi Eng.Steven D.M.Mlote,Mwenyekiti wa Makandarasi,Eng.Pfrof.Ninatubu Lema,Waziri wa Ujenzi Mhe.John Magufuli ,Hakimu Mkazi Mhe.Verynice Kawishe na Wakili Mkuu wa Serikali (PSA) Mhe.Donald L.Chidowu.
 Naibu Waziri wa  Uchukuzi,Mhe. Eng.Dkt.Charles Tizeba akipongezwa na Mhe. Dkt John Magufuli mara baada ya kuapishwa.
 Wahandisi viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mkazi   Mhe.Verynice Kawishe wakati akiapisha Wahandisi 120 kwa pamoja.
 Wahandisi wakiwa wanaapa kwa pamoja.
 Wahandisi wakiwa wanaapa kwa pamoja.
 Wahandisi wakiwa katika picha ya Pamoja kwa makundi manne tofauti mara baada ya kula  kiapo cha uaminifu katika kazi yao ya Uhandisi.

at Sunday, May 25, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Familia ya bwana Sijaona Simon wa Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mzazi ndugu Simon Malosha kilichotokea siku ya alhamisi tarehe 22/5/2014 saa nane mchana katika hospitali ya TMJ. 

Mazishi yatafanyika jumapili tarehe 25/5/2014 saa tisa mchana katika Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. Misa ya kumuaga marehemu na kutoa heshima za mwisho, itafanyika kwa Marehemu Sijaona magorofa ya Urafiki block QA. 

Taarifa ziwafikie kaka yake mkubwa William Lukuba wa Nyakato Mwanza, Dada yake mkubwa wa Mwanza, waumini wote wa Kanisa la Mlima wa Moto Dar es Salaam ndugu, jamaa na marafiki wote wanao husika na msiba huo.

at Sunday, May 25, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments


 Baadhi ya washiriki wa mchezo huo wakifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa shindano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Magunila  Kihonda Mjini Morogoro.
 Wahsiriki wa shindano hilo kutoka mikoa mbailimbali wakiwa katika ukumbi  huo wakishuhudia pambano hilo.

 Irene Kihupi mchezaji kutoka mkoa wa Dar es Salaam akiwa katika pambano hilo.
 Joyce Laize mchezaji kutoka mkoa wa Arusha akiwa katika pambano hilo.
 Mwenyekiti huyo wa Dats akizindua mchezo huo ili kuruhusu pambano kuanza rasmi.
 Baadhi ya wachezaji wakiwa katika pambano hilo
Frolida Namajojo katibu wa Dats mkoa wa Morogoro akiwa katika mazoezi kabla ya kuanza mchezo huo.

at Sunday, May 25, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 
MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi Tanzania, Amina Ngaluma, amezikwa jana mchana katika Makaburi ya Kitunda Machimbo, jijini Dar es Salaam, kuashiria kuwa sura au sauti ya mkali huyo haitasikika wala kuonekana tena ana kwa ana.
 
 
Kwakheri Amina Ngaluma, mwili wake ukiingizwa kaburini jana mchana, katika makaburi ya Kitunda Machimbo, jijini Dar es Salaam.
 
Ngaluma aliyefariki nchini Thailand, aliletwa jana usiku, ambapo wadau na mashabiki wa muziki wa dansi Tanzania, walipata fursa ya kushiriki katika mazishi yake.

Tofauti na wakati wa mapokezi ambapo wanaamuziki walishindwa kuhudhuria, jana katika mazishi hali ilikuwa nzuri kwa wadau wengi kujitokeza.

at Sunday, May 25, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

LEO, jumapili ndio Arobaini ya Mwanamuziki mkongwe, Marehemu Mzee Muhidin Gurumo maarufu kama Mjomba au Kamanda, aliyefariki yapata mwezi mmoja uliopita ambapo shughuli ya arobaini ya Gurumo itaanza saa saba mchana, nyumbani kwake Mabibo External. 

Wadau wote bila kusahau mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi Tanzania, wanaombwa kufika ili kuendeleza dua kwa mzee Gurumo. Shughuli ilipaswa kufanyika jana Jumamosi, ila ilisogezwa mbele ili wadau hao wapate kushiriki pia mazishi ya marehemu Amina Ngaluma aliyezikwa jana.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Jumla ya Waandishi wa Habari 10 wamefanikiwa kufikia hatua ya fainali ya Tuzo za Uandishi wa Habari za Shirika la Hifadhi za Taifa za mwaka 2013.


Wanahabari waliofanikiwa kufika hatua ya fainali ni pamoja na Frank Leonard (Habari Leo), Jackson Kalindimya (Nipashe), Humphrey Mgonja (Radio SAUT FM), Raymond Nyamwihula (Star TV) na Vedasto Msungu (ITV).


Wengine ni pamoja na Kakuru Msimu (Star TV), Gerald Kitabu (The Guardian), Salome Kitomari (Nipashe), David Rwenyagira (Radio 5) na Cassius Mdami (Channel Ten).


Hafla ya utoaji Tuzo za Habari za TANAPA itafanyika siku ya Jumanne tarehe 27 Mei, 2014 jijini Mwanza ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.


Hafla hii itaenda pamoja na Mkutano wa kila mwaka baina ya TANAPA na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini inayotarajiwa kuanza wiki ijayo jijini Mwanza.


Jumla ya kazi zilizotumwa kwa ajili ya kushindanishwa mwaka huu ni 114 tofauti na kazi 34 za mwaka jana. Ongezeko hili la asilimia 235 lililazimu Jopo la Majaji kutumia muda mwingi zaidi wa kupitia kazi zote na kupata washindi. Kati ya kazi 114 zilizotumwa, kazi zilizohusu Uhifadhi ni 64 (sawa na 56%) na kazi zilizohusu Utalii wa Ndani zilikuwa 50 (sawa na 44%). Tuzo za Uandishi wa Habari za TANAPA hutolewa kila mwaka kwa nia ya kuwashirikisha wanahabari kushindanisha umahiri wa kazi zao katika kuelimisha jamii umuhimu wa dhana ya Uhifadhi kwa maeneo yaliyotengwa kisheria kama Hifadhi za Taifa na uhamasishaji wa Utalii wa ndani kwa faida ya uchumi wa nchi yetu.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
23.05.2014

at Friday, May 23, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta akijibu hoja za wabunge kabla Bunge halijapitisha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015.
Maofisa wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wakiwa pamoja na Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakifuatilia kikao cha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa 
Mwaka 2014/2015.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Joyce Mapunjo mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2014/2015.
Wabunge wa Afrika Mashariki wakiwasili Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa kuteuliwa Mhe.James Mbatia akifurahia jambo na Mhe.Shyrose Banji Mbunge wa Afrika Bunge la Afrika ya Mashariki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Joyce Mapunjo (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mhe.Samia Suluhu (kushoto) na Mhe.Celina Kombani.
Mbunge wa Chalinze,Mhe.Ridhiwani Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki,Mhe. Shyrose Banji 
Wanachuo kutoka Chuo cha Mipango Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja nje ya viwanja vya Bunge wakati walipofanya ziara ya kimafunzo Bungeni na kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015.
Wanachuo kutoka Chuo cha Uuguzi Mirembe Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya viwanja vya Bunge wakati waliofanya ziara ya kimafunzo Bungeni na kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015 .
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ,Joyce Mapunjo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa wa wizara yake pamoja na Wabunge wa Afrika ya Mashariki mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015.

at Friday, May 23, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Olabisi Ibidun Cole, raia wa Nigeria akiwa na kete 82 za madawa ya kulevya 

Mwandishi wetu, Dar es salaam
Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Cole alikamatwa Jumatatu akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Alfred Nzowa zimesema pamoja na mbinu zake na kujiamini, mwanamke huyo alikamatwa kutokana na ushirikiano wa vitengo mbalimbali vya uwanja wa ndege.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema mwanamke huyo alikamatwa Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
Selemani alisema raia huyo aliwasili nchini Mei 15, mwaka huu na alikaa muda wote bila ya kuwa na shughuli yoyote, jambo ambalo lilitiliwa shaka na kumkamata.
“Huyu mwanamke achana naye, akisimama mbele yako huwezi ukaamini kwa jinsi anavyojiamini. Alikuwa na mbinu mpya ya kufunga hizo kete. Kila moja ilifungwa kwa karatasi inayofanana na ganda la sigara,” alisema Selemani.
Alisema mwanamke huyo alitumia mbinu hiyo ili asigundulike wakati akikaguliwa kwa mitambo maalumu inayogundua dawa za kulevya.
Taarifa zaidi zinasema kuwa kutokana na mbinu yake ya ufungaji wa kete, mwanamke huyo alikuwa tayari amevuka hatua ya kwanza ya ukaguzi.
Nzowa alisema baada ya kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa aliingia nchini kwa ajili ya kutafuta soko la kuuza vipodozi na nguo.
“Wakati tukiendelea kumhoji, Kikosi Kazi cha Kuthibiti Dawa za Kulevya kilibaini na kugundua kuwa alikuwa amemeza dawa za kulevya.
“Huyu ni mzee, lakini tumeshangaa kuona bado ana nguvu za kutosha na tulishangaa baada ya kutoa kete 20 kwa mara moja katika awamu ya kwanza, jambo hili si rahisi kutokana na umri wake,” alisema Nzowa.


Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na hati ya kusafiria ya Nigeria, anaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
SOURCE:MWANANCHI