MJEMA BLOG

JICHO LA MWANDISHI

  • RSS
  • Delicious
  • Digg
  • Facebook
  • Twitter

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Rufaro Chatora (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa kuboresha ushirikiano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Shirika la Umoja wa Mataifa nchini UN lakutana na wanahabari kujadiliana na kudumisha ushirikiano wao katika habari ambapo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wamekuna na viongozi mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ili kujadili kwa pamoja.
UN wameeleza kazi zinazofanywa na shirika hilo ili waweze kushirikiana kwenye mambo mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, elimu na kuzifahamu kazi za mashirika hayo hapa nchini.

Hivyo waandishi na wahariri wa habari wameombwa kudumisha ushirikiano katika kazi zote zinazofanywa na mashirika yanayosaidia nchini kwa kiasi kikubwa. Pia wameweza kuzungumzia ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka kwa kasi sana hivyo kuwataka kuweza kuandika habari zinazowajuza jamii ili kuweza kuuepuka.

Nia na madhumuni ya mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari ni kuweza kujenga ushirikiano madhubuti baina yao na kuweza kushirikiana kwa karibu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wahiriri wa vyombo vya habari nchini ambapo alielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ikiwemo utekelezaji wa agenda mbalimbali za malengo ya milenia.
Bwana Clioni akiendesha mjadala baina ya viongozi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akitoa salamu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati wa mkutano wa kuendeleza ushirkiano baina ya Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari nchini.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akitoa shukrani kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati walipokutana na wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuboresha ushirikiano na mahusiano baina yao.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha mkutano huo baina ya Umoja wa Mataifa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kuboresha mahusiano baina yao na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Untitled
Mkutano ukiendelea huku wengine wakipitia makabrasha mbalimbali yenye taarifa za Umoja wa Mataifa.
Mmoja wa wahariri akihoji swali kwa viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa wakati wa mkutano huo.
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuboresha mahusiano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mashirika ya umoja wa mataifa nchini.
 

SAM_0783
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea ajali ya moto kwa ajili ya kukabidhi misaada.

Na Daniel Makaka, Sengerema

NAIBU Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Misaada aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.

Akikabidhi misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione namna ya kuwasaidia.

SAM_0723
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akiwa ndani ya boti kuelekea kukabidhi misaada katika kisiwa cha Nyamango jimboni kwake.

.....Serikali itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni misaada tu.
Awali Katibu wa kamati ya maafa wilaya Sengerema Bw. Benard Myatilo akitoa taarifa ya wahanga wa tukio hilo alisema kuwa matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo Septemba 19 majira ya saa nane usiku kaya 40 ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa Kibatari ndani ya nyumba na tukio la pili kaya 11 kuezuliwa na mvua ilyoambatana na upepo likiwemo jengo la kanisa Katoliki kisiwani humo.

Pia alisema kati ya wahanga hao hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo licha mali zote zlizokuwemo kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba hazina mahali pakuishi huku zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na jamaa wanaoishi katika kisiwa hicho.

SAM_0749
Muonekano wa baadhi ya nyumba zilizoteketea kwa moto katika kisiwa cha Nyamango wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

SAM_0750
SAM_0753
Kanisa la Roman Katoliki katika kisiwa cha Nyamango lililoezuliwa na upepo ulioambatana na mvua.
SAM_0775
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba (mwenye suti ya kijivu) akikabidhi misaada ya mablanketi 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Bitulo (kulia kwa naibu waziri) huku Mwenyekiti wa CCM tawi la Nyamango, Japhet Kafula akishuhudia tukio hilo
 

The newly expected couple Richard Miller and Kara Lee from America poses in a picture at Shira Cave point shortly before descending to a place where they exchanged vows in Mount Kilimanjaro yesterday.


Chief Park Warden for Kilimanjaro National Park Erastus Lufungulo (right) and TANAPA’s Corporate Communications Manager Pascal Shelutete (second left) poses in a picture with the newly expected couple at Shira Cave point shortly before they exchanged vows in Mount Kilimanjaro.


 It was not easy an easy task for this couple as seen here in a red and black jacket far behind passing across hard rock on Mount Kilimanjaro when they were heading to their wedding venue.

The newly expected couple arriving at the venue of their wedding in Mount Kilimanjaro. Here the newly expected couple was seen more than happy, as they were about to fulfill their long dream of getting married in Mount Kilimanjaro.
Choir of St. Clara from Moshi was there to deliver Christians wedding songs during the holly wedding service in Mount Kilimanjaro.
Pastor Aloyce Mbugi (right) from TAG Arusha Victory Christian Centre reading a word of God during the holly wedding service in Mount Kilimanjaro.  Left is Mr. Isaya Mwashala who was an interpreter.


 The newly expected couple sitting together with their Patron Ansigar Mtandika and Matron Neema Njau.


The groom Richard Miller is seen putting a wedding ring to the bride Kara Lee in Mount Kilimanjaro.
Managing Director of Zara Tours Company Zainab Ansell who organized the tour of the newly expected couple is seen here happy with the couple in Mount Kilimanjaro.

Kigaila akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila akionesha barua za kuomba vibali vya kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini. 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesisitiza kuwa migomo na maandamano yasiyokoma nchi nzima yapo palepale na kwamba yanaanza rasmi leo kwa kishindo kikubwa na hakuna mtu wa kuyazuia kwani ni haki yao kikatiba.

Chadema kimesema lengo la maandamano hayo ni kuishinikiza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitoe tamko la kusitishwa Bunge Maalum la Katiba linaloendelea mjini Dodoma huku likifuja fedha za wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Organizasheni na Mafunzo wa chama  hicho, Benson Kigaila wakati akizungumza na wanahabari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni.

"Maandamano yaliyotangazwa na Freeman Mbowe si ya kwake ni maazimio ya Mkutano Mkuu wa Chadema uliofanyika Septemba 14, mwaka huu.

"Tunasisitiza kuwa maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima yapo palepale, lengo letu ni kuishinikiza Serikali isitishe Bunge la Katiba kwani  mkutano mkuu uliazimia jambo hilo baada ya kuona kuwa kinachofanyika Dodoma hakitatupa Katiba Mpya, bali fedha za wananchi zinatafunwa bure"alisema.

Aidha, alisema maandamano yao yapo kisheria ambapo katika Katiba ya nchi,  maandamano ni haki sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 11 kifungu kidogo cha 1 inaruhusu jambo hilo.

Kigaila aliongeza kuwa sheria hiyo inataka waandamanaji kutoa taarifa ndani ya saa 48 kabla ya na si kuomba kibali taratibu ambazo wao wameshazipitia.

"Natoa mwito kwa Watanzania wote wakatae ufisadi unaofanywa na Bunge Maalumu la Katiba. Kilichoko Dodoma ni kumaliza fedha ambazo zingetumika kujengea nyumba za walimu au hata zahanati katika maeneo mbalimbali nchini,"alisema .

Kigaila alisisitiza kuwa wamepata barua kutoka Jeshi la Polisi kuwataka kusitisha maandamano lakini hawatasitisha kwa sababu, sababu za katazo hazina mashiko na hazijanukuu kifungu chochote cha sheria.

Alisema licha ya wao Chadema, maandamano yao hayo yamepata baraka kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Mkurugenzi huyo wa organizasheni wa chama hicho alisema maandamano hayo yanafanyika katika ngazi ya majimbo, wilaya na mkoa, ambapo kwa mkoa yataanzia maeneo tofauti kuishia ofisi za mkuu wa mkoa husika na kwa wilaya yatakwenda kwa mkuu wa wilaya husika.

Alisema maandamano hayo kila mahali yataanza asubuhi, huku kwa mikoa mitatu ya kanda ya Dar es Salaam yataanza keshokutwa Jumatano.

Kwa upande wale Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya alisema sababu nyingine iliyotolewa na polisi kuwa maandamano  hayawezi kufanyika kwa sababu kesi iliyofunguliwa Saedy Kubeinea ya kupinga Bunge hilo ipo mahakamani kuwa  haina mashiko kwa kuwa Chadema ni taasisi inayojitegemea na inamaamuzi yake ya kichama.

at Monday, September 22, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

Na Benedict Liwenga na Magreth Kinabo.

RASIMU ya Katiba  Mpya  iliyopendekezwa inatarajiwa kuwasilishwa  katika Bunge Maalum la Katiba Septemba 24, mwaka huu.

Mabadiliko hayo yametangazwa leo jioni na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahya Khamis Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Aidha Katibu huyo amesema uamuzi wa mabadiliko hayo, umetokana na kufanyika kikao baina ya Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi. 

Hata hivyo Katibu huyo amesema kuwa kazi ya uandishi wa Rasimu hiyo imeshakamilika na kazi iliyobakia ni kuipitia kwa makini, hali iliyosababisha mabadiliko ya uwasilishaji wa Rasimu hiyo katika Bunge hilo, uliopangwa kufanyika hapo kesho Septemba 22, mwaka huu.

“Uwasilishwaji wa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa sasa utafanywa siku ya Septemba 24, mwaka huu, ” alisema Katibu wa Bunge hilo.

“Kamati ya uongozi imeona kuwa ni busara na kupewa siku mbili kwa ajili ya kuipitia upya ile kazi ambayo wameifanya ili kufikia tarehe 24 kutoa kitu makini, napenda niwahakikishie wananchi kuwa kitu kizuri kinakuja.

Aliongeza kuwa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo, inatarajia kukabidhiwa Rasimu ya Katiba Mpya iliyopendekezwa tarehe 23 Septemba, mwaka huu kutoka kwa Kamati ya Uandishi wa Bunge hilo.

Aidha, Katibu huyo ameeleza sababu ya uairishwaji wa uwasilishwaji wa Rasimu hiyo Bungeni hapo kutokana na ugumu, umakini na uzito wa kazi yenyewe.

“Tulikuwa tumepanga hapo tokea awali kufanya kikao na Kamati ya Uongozi asubuhi tukafanya mchana na hata jioni kila wakati Kamati ya Uandishi ikawa bado haijamaliza hiyo kazi na tulivyofanya kikao cha Kamati ya Uongozi hii jioni tukamuita Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi akaonyesha kwamba hiyo kazi walikuwa wakiifanya usiku na mchana na hadi sasa wamesema wamemaliza kuandika.

“Lakini kutokana na namna walivyokuwa wakiifanya hiyo kazi kwa uharaka na ingawa walikuwa wakiifanya kwa umakini lakini wanahitaji muda wa kuanza kuipitia kwa makini zaidi kuanzia mwanzo mpaka mwisho hivyo wakaomba wapewe muda wa siku mbili ya kesho na keshokutwa ili kuweza kuipitia kazi hiyo kwa umakini,”alisema.

Katibu wa Bunge hilo, aliongeza kwamba mabadiliko hayo hayataweza kuathiri upigaji kura uliopangwa kufanyika Septemba  29  hadi 2 Oktoba mwaka huu.

“Tumeacha  siku ya Septemba  29, mwaka huu  ili iwe siku ya kuanza kupiga kura na tumalize 2 Oktoba, mwaka huu ili tuhakikishe kwamba Oktoba  4 , mwaka tumemaliza hili zoezi,” alisisitiza.

Aidha Katibu huyo alifafanua kuwa ratiba kuhusiana na masuala hayo  ataitoa kesho.

at Monday, September 22, 2014 Posted by Daniel Mjema 0 Comments

DSC_0007
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuhudhuria maadhimisho hayo na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi (wa pili kulia), Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala (katikati) na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania , Bw. Ali Rajab (kulia) pamoja na viongozi wengine taasisi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinizim). 

 Na Mwandishi wetu
WAKATI Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon anahimiza serikali duniani kutafuta chanzo cha kukosekana kwa amani na kuongezeka kwa watu wenye misimamo mikali, wasemaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa amani Duniani wameitaka serikali ya Tanzania kutupia macho makali mauaji ya albino nchini.

Akimwakilisha Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika adhimisho lililofanyika viwanja vya Mnazi mmoja leo Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Alvaro Rodriguez, alisema ili kudumisha amani kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyiwa kazi hasa kutambua chanzo cha migogoro inayosababisha msuguano mkubwa katika jamii na kukosekana kwa amani.
Alisema amani ina maana kubwa kwa jamii na ndio maana Umoja wa mataifa miaka 13 iliyopita iliamua kuadhimisha siku hiyo kwa lengo la kushawsihi makundi yanayosigana kupata nafasi ya kuzungumzia na kuona maana ya amani.

Alisema pamoja na kuwepo kwa hatua kubwa tangu kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kuadhimisha amani, safari ya kufikia amani ni ndefu na ili kufanikiwa pande zote ni lazima kwenda hatua kwa hatua kwa kushirikiana.

Alisema mafanikio ambayo yamepatikana ni pamoja na UN kufanikiwa kufundisha kada ya habari juu ya uandishi katika mazingira tete na kusaidia majadiliano ya kitamaduni yanagusa masuala ya amani.

DSC_0031
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (katikati) akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay. Aidha alisema kwamba wanafanyakazi na Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha kwamba wanastawisha mipango yote inayolenga kuzuia ghasia na kuboresha mipango inayoimarisha amani.

Akihutubia bada ya mashuhuda kuzungumzia hali ya tishio la amani nchini Tanzania hasa la kukosekana kwa amani miongoni mwa watu wenye ulemavu wa ngozi albino, Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa aliipongeza serikali ya Tanzania kw ajuhudi zake za kuimarisha amani katika kanda ya maziwa makuu na kushiriki katika operesheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa ziliziolenga kuleta hali bora zaidi ya maisha kwa watu wanaoishi katika hekaheka za kivita.

Akiwa na mwezi mmoja tangu awalisili nchini mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa nchini amesema kwamba anatarajia kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali na wananchi wa Tanzania kuhakikisha taifa la Tanzania linaendelea kuwa na amani Wakati Mwakilishi huyo amesema kwamba watu wengi duniani wanawaonea gere wananchi wa Tanzania kwa amani waliyonayo, mwakilishi wa Under the Same Sun, Vicky Ntetema ametaka kupitiwa upya kwa sheria ya uchawi ya mwaka 1928 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2002 ili kukabiliana na mauaji ya albino nchini ambayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na waganga wa kienyeji.

DSC_0039
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid meza kuu.

Alisema sheria hiyo ina mwanya mkubwa wa wauaji kucheza nayo na kusababisha sehemu kubwa ya kesi zilizopo kushindwa kuwatia hatiani wahusika. Alisema wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu mauaji ya albino na ukataji wa viungo umeongezeka.

Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 25 za afrika zinazofanya ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi, toka mwaka 2006 watu 74 wameuawa, 56 wamenusurika na 11 wameongezewa ulemavu huku makaburi 18 ya albino yakinajisiwa kwa kufukuliwa.

 Watu wa kituo cha haki za binadamu wamesema pamoja na kuwepo na matukio 120 ya ukatili dhidi ya albino kesi 11 tu ndio zilizofikishwa mahakamani huku tano zikiwa zimekatiwa hukumu ambazo hazijaridhisha. Vicky alisema katika matukio yote hayo chanzo ni ushirikina lakini kutokana na kukosekana zimeshindikana kuzimaliza zinavyotakiwa.
DSC_0082
Brass band ya jeshi la Magereza ikiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho hayo jana.

Vicky aliitaka jamii kuwalinda albino kwani serikali pekee haiwezi kufanya kitu chochote huku akisema kwamba hesabu ya albino mmoja katika kila wananchi 1,400 haiwezi kulindwa kwa dhati na serikali kutokana na idadi ya polisi kutokua sawa na wananchi. Aidha alishauri serikali kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika kabla ya kuingia mahakamani ili waweze kusimulia vyema kadhia zao na pia wasiangushwe na wanasheria ambao wanatumia udhaifu wa kisheria kuwatoa watuhumiwa hatiani.

Pamoja na Vicky Ntetema kushawishi wananchi kulinda albino na kuwafichua wauaji Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya ameitaka serikali kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata utulivu wa kutosha kuendelea na shughuli zaka na kuhimiza mahakama kutenda haki.

Aliwakumbusha wananchi kama alivyosema Sydina Omar kwamba kila mmoja ataulizwa amefanya nini kukomesha madhila katika jamii wakati wa kiama na kusema serikali isipowajibika itasema nini na wananchi nao pia watajibu nini.
DSC_0100
Pichani ni baadhi wadau kutoka taasisi mbalimbali pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja huku wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha amani nchini na kupinga mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar.

Alisema amani hailetwi kama mvua , inatafutwa na kusema watu wasipotafuta amani na kuhakikisha amani inakuwapo itakuwa shida kubwa kwa taifa hili ambalo miaka yote limeogelea katika bahari ya amani.Aliwasihi waumini wa Kiislamu na wananchi wengine kuhakukisha kwamba amani inakuwa ajenda ya kudumu kila wanapokutana pamoja.

Katika maadhimisha hayo ambapo wananchi walianza maandamano shule ya Uhuru Mchanganyiko hadi viwanja vya Mnazi mmoja, mgeni rasmi Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk Seif Rashid alisema serikali imejipanga kuhakikisha inakomesha mauaji ya albino na kuwataka wananchi kuisaidia kwa kutokuwa waoga kutoa ushahidi na pia kuwaripoti watuhumiwa.

Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ya haki ya amani kwa watu wote, komesha mauaji ya albino inahamasiaha umma wa Tanzania kulaani,kukemea na kukomesha mauaji kwani yanakwenda kinyume na katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 14 ambayo inaeleza kwamba kila mtu ana haki ya kupata hifadhi katika jamii.Aidha waziri alitaka kutekelezwa kwa agizo lake kuhusu tiba mbadala na za asili na kusema serikali itaendelea kulinda amani na kutoa ulinzi kwa wathirika.

DSC_0108
Meza kuu ikipoeka maandamano ya siku ya kimataifa ya amani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
DSC_0248
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Mh. Seif Rashid (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala, Balozi wa Uturuki nchini, Mh. Ali Davutoglu.
DSC_0593
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid, akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
DSC_0415
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
DSC_0418
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipongezwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu baada ya kusoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
DSC_0279
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akisoma risala yake kwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
DSC_0284
Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alilaani vikali mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinizim) na kusema kuwa watu wote wanaoshiriki katika mauaji hayo kamwe hawatoiona Pepo ya Mwenyezi Mungu.
DSC_0384
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba wa umoja wa mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
DSC_0300
Baadhi ya wadau kutoka taasisi na asasi mbalimbali nchini walioshiriki kwenye maadhimisho hayo.
DSC_0420
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay akitoa nasaha kutoka kwa Tume hiyo, ambapo alitoa rai kwa mtu yeyote yule ambaye ana malalamiko au matatizo katika Haki za Binadamu anakaribishwa kwenye tume hiyo kwa ajili kupata msaada wa kisheria.
DSC_0519
Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.
DSC_0534
Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
DSC_0540
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.

5Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali mwenyekiti wa kikundi cha Mbagala Youth Group Said Mponda baada ya kuzipokea kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC ambalo limetoa mashine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana mashine hizo zilikabidhiwa kwa mkuu wa wilaya na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC tawi la Temeke Bw. Wencenslaus Tillya. 


3Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akipokea mashine za kufyatulia matofali kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Wilaya ya Temeke Bw. Wencenslaus Tillya ambazo zilikabidhiwa kwa vikundi vya vijana wilayani humo.
 
4Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine kwa mwenyekiti wa kikundi cha Sokoine Youth Development William Gabriel.
6Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali mwenyekiti wa kikundi cha Chang'ombe Youth Development Eunice Mlwale baada ya kuzipokea kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC 
8Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali mwenyekiti wa kikundi cha Chapakazi Youth Youth Nathanaeli Daniel Kidaila baada ya kuzipokea kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC. 
9Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akiwa katika picha ya pamoja na vikundi hivyo mara baada ya kukabidhi mashine za kufyatulia matofali kwa vikundi vya vijana vya Temeke ambazo zimetolewa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Wencenslaus Tillya Meneja wa NHC Temeke na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana. Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba NHC na baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke. 

11